Swahili
Home » Mgombea wa chama cha Green Dkt.Frank aahidi wanajeshi maisha bora
HABARI MPYA SIASA

Mgombea wa chama cha Green Dkt.Frank aahidi wanajeshi maisha bora

Dkt.Frank ambaye ni mgombea wa chama cha green amekuwa akiendesha kampeni yake ya kusaka kura kwenye wilaya ya Nyabihu ambako amepokewa kwa shangwe na anasema amekuwa na kampeni nzuri ukilinganisha na mahali pengine alipopitia.

Mgombea huu alikaribishwa na katibu mtendaji wa tarafa ya Shyira Niyibizi Louis, ambaye amesema

“ Mkae mfike hapa ni salama ila mnaona tunazunguukwa na milima. Mchukue muda huu wa kuwaelezea wananchi mipango yenu kwa kuwa ndio watakao kuwa na uamuzi wa kumchagua yeyote wanayemwona anafaa”

Frank akieleza mipango yake

Alipokuwa akieleza mipango yao kwa wananchi alichukua muda muhimu akieleza kuhusu tatizo la mshahara mdogo kwa baadhi ya wafanyakazi wakiwemo mwalimu, majeshi na polisi japokuwa wana umuhimu sana kwa maisha ya nchi. Amesema kutaweka miradi mingi ya kuboresha maendeleo yake na kuwaongezea mishahara na hata  mradi wa miliki nyumba”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Aliendelea kusema kwamba kutajengwa nyumba za kifari zikewe madarasa na hospitali hadi maisha ya mwanajesh  na familia yake ageuke kuwa bora. Unamkuta mwanajeshi akishinda miezi kadhaa bila kuikuta familia yake kwa sababu huwa wanaishi mbali nayo kwa mfano akiwa anafanya kazi yake Musanze, Nyabihu na familia yake ikiwa inakaa Kigali.

Kuhusu kodi mgombea huu amesema kwamba hataki watu ambao wanaihama nchi kwa kuogopa uzito wa kodi. “Tutakuwa kama India ambako wana Kodi moja kwa hivyo tutaweka kodi moja kwa bidhaa na hii italingana na thamani yake na hivyo tuepukane na ile tabia ya kuwafanya wananchi kuihama nchi kwa sababu ya kuogopa kodi wala siyo mzozo wa kisiasa ila hali ya usalama mbaya.

Ameahidi kuwa wakati ambapo watampa kura atakuwa akija kuwazuru wala si kukaa Ofisi mjini Kigali bila kujua yanayoendelea kijijini.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com