Swahili
Home » Mgombea Mpayimana Phillipe kuweka mfumo wa kuzaa watoto watatu
HABARI

Mgombea Mpayimana Phillipe kuweka mfumo wa kuzaa watoto watatu

Mpayimana Phillipe ambaye ndiye mgombea huru pekee miongoni mwa wagombea watatu wanaowania kiti cha urais wa Rwanda amekuwa kwenye akiendesha kampeni zake kwa siku ya nane kwenye wilaya za Rubavu na Nyabihu.

Alipokuwa akieleza mipango yake kwa wananchi wa Rubavu na Nyabihu amesema kwamba ataweka mfumo wa kutozidi watoto watatu.

Amesema kuwa mfumo wa kuzaa watoto ambao mtu ana uwezo wa kuwalea utageuka kuwa kuzaa ambao nchi itaweza kuwalea.

Anaendelea kufafanua kwamba kulingana na mipango yake mwanamke ndiye atakaye kuwa chanzo cha utekelezaji wa mfumo huu kwa kuwa ataweka utaratibu wa kudhibiti uzazi wao ili kusiwe na yeyote atakayezidi watoto watatu.

Mgombea huyu ambaye ndiye mgombea pekee anayewania kiti cha urais wa Rwanda anaendelea na ziara za Kampeni yake ya kuwaelezea wananchi mipango yake ili waje wakampa kura katika uchaguzi wa hapo mwezi ujao.

Mpayimana amekuwa akilalamika kukumbwa na matatizo yanayohusu uwezo mdogo wa kifedha unaofanya kutoendesha kampeni zake ipasavyo ila mpaka sasa angali anaendelea kufanya kampeni zake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakati anapoendesha kampeni mgombea huyu huwa ana wananchi wachache sana wanaohudhuria kampeni zake na viti vichache vinavyoandaliwa huwa wazi kwa sababu wananchi wanafikiri vimeandaliwa kwa ajili ya waheshimiwa.

Kampeni za wagombea zitaendelea hadi tarehe 3 Agosti ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuendesha kampeni kwa wagombea kukisalia siku moja uchaguzi ukafanyika. Mpayimana naye anatarajiwa kutembea wilaya zote za nchi akieleza mipango yake kabla ya tarehe hiyo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com