Swahili
SIASA

Mgombea Frank amekuwa wilaya ya Ngoma ambapo aliahidi kupambana na maswala yanayowakumba raia.

Dkt.Frank alikuwa kwenye wilaya ya Ngoma ambapo amekuwa akiendesha kampeni yake ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi ujao na kuwaahidi watakaomchagua mengi yaliyomo kuondoa kodi ya mashamba, kupanda mimea ya matakwa ya wananchi na mengine ikiwemo kupambana na tatizo la ukosefu ajira kwa vijana.

Kampeni ya Dkt. Frank iliendeshwa ambayo iliendeshwa kwenye wilaya ya Ngoma, tarafa la Kibungo ilionekana kuhudhuriwa na raia wengi ikilinganishwa na wale waliohudhuria alipokuwa kampeni kwenye wilaya ya Kirehe.

Alipokua akieleza mipango yake kwa waliohudhuria amesema

“usalama wa kwanza ni wa chakula na ndio sababu mara tu baada ya uchaguzi maswala kama kodi ya mashamba na kutopanda mbegu ya matakwa ya wanchi hayatakuweko kamwe mwezi Septemba ikiwa mtanipa kura”

Kama alivyozungumzia kwenye kampeni zake za awali Dkt. Frank anapanga pia kukuza sekta ya kilimo kwa kuwaacha wakulima kupanda mbegu za chaguo lao siyo siyo kuwashurutisha mbegu maalum za kupanda.

Hapa aligusia kuhusu maeneo yanayo na mazao mengi ya ndizi na kuahidi kwamba atawaletea mimea yenye uezo wa kakabili mazingira maalum kwa ajili ya kupambana na njaa.

Wananchi ambao walihudhuria hafla hiyo walionyesha hali ya kusisimka na kuahidi kumaliza kazi muda wa kura utakapowadia.

Mgombea huyu aligusia pia matatizo anayokumbana nayo katika shughuli zake za kampeni ikiwemo kutohudhuria kwa wingi kwa wananchi, kuvurugiwa kampeni na wananchi, kubadilika badilika kusiko na mpango na kuonyeshwa kutofurahiwa kwa viongozi wa ngazi za nchi za uongozi.

Dkt. Frank hakukosea pia kueleza kwamba swala la ukosefu kazi linalowakumba vijana yeye atalitolea suluhu kwa kuwasaidia kutajitafutia kazi, kwa kufuta kodi zinazowasumbua wananchi katika shughuli za kujiendeleza kama kodi ya mashamba na hata nyongeza ya mshahara kwa askari wa jeshi na polisi kwa sababu ya uzito wa kazi wanayoifanya.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com