kwamamaza 7

Mgawanyiko wa bajeti katika Nchi za Afrika ya Mashariki

0

Wanashirika wote wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki wanatakiwa kutangaza bajeti zao nyakati moja ili kuilinganisha na matakwa ya ushuru.

Tarehe 8 juni nchi kama Tanzania, Rwanda na Uganda zilitangaza bajeti zao, huku Kenya ikiwa ilikwisha tangaza yake hapo Machi kwa ajili ya kuilinganisha na maandalizi ya kura za urais yanayotarajiwa kupigwa hapo Ogasti. Hata hivyo nchi ya Sudani Kusini yaijatangaza Bujeti yake pomoja na Burundi ambayo kwa nadra huheshimu masharti haya.

Rwanda miongoni mwa nchi zenye bujeti ndogo

Kulingana na takwimu za mwaka jana ,Sudani Kusini ndio iliyokuwa na bujeti ndogo yeni dola za Kimarekani 193 isipokuwa Burundi ambayo haikutangaza bujeti yao mwaka huo.

Takwimu za leo zinaonyesha kwamba Rwanda itatumia bujeti ndogo ukulinganisha Na nachi kama Uganda Tanzania na hata Kenya.

Kenya ndio inayoongoza kwa wingi wa fedha zitakazotumiwa ikiwa itatumia dola zipatazo billioni 25 na millioni 169 huku Tanzania ikitumia dola billion 14 na millioni 21 kulingana na billion 13 na million 500 za mwaka jana zilizotumiwa mwaka, Uganda inafuata na billion 8 na millini 9 za dola za kimarekani,ikwa ilikuwa billion 7 na million 900 za dola mwaka jana.

Rwanda kwa upande wake itatumia dola billioni 2 na million 540 za dola za Kimarekani.

Inakisiwa kuwa Burundi nayo itatumia dola million 767, 200,311 kwa mjibu wa tovuti ya Ikiriho, kwa kinyume na habari zilizotangazwa na Daily Monitor iliyotangaza kwamba Burundi watatumia bujeti ya billion 17 ambazo zote zitatoka nje ya nchi.

Mishahara na shughuli za kawaida za serikali kuchukuwa fedha nyingi

Katika bujeti ya mwaka huu ambayo ni sawa na million 2,094.9 za dola za kimarekani yenye ongezeko la millioni 140 yaani 7% kulingana na mwaka jana. Inaonekana kwamba shughuli za kawaida za serikali zitagharimu 54 % ya bujeti yote.

Inaonekana kwamba katika fedha zitakazotumiwa na serikali 66% yake atatokea kwenye mapato ya ndani ya nchi yaani billioni moja na millioni 375.

Rwanda itatumia kwa jumla ya 83% ya bujeti yote kutoka mfuko wake huku 17% ikiwa ni misaada.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alipokuwa akitangaza bajeti hii Amb. Claver Gatete alisema kuwa billioni 52,9 zitatumiwa kuongeza mapato ya bidhaa zinazotumwa nje ya nchi.

Uchukuzi wa watu na vitu utachukua 248.5 billioni za faranga za Rwanda, Kilimo 110,5. Sekta ya nishati itatumia billion 84 ikiwemo kusambaza umeme kwa wananchi.

Katibu wa serikali wa wizara ya Uchumi ya Kenya, Henry Rotich, alitangaza mwezi Machi kwamba bajeti ya 2017/2018 itatilia mkazo ongezeko la miundombinu, ikiwemo barabara na ongezeko la mapato ya kilimo na kadhalika.

Waziri wa uchumi wa Tanzania Philip Mpango aliwaambia wabunge kwamba GDP ya nchi inaizidi ya nchi zote zingine za Afrika ya Mashariki kwa kuwa shilingi halikudhorora. Alikiri kwamba kiwango kingi kitatumiwa kwa sekta ya miundombinu.

Waziri, matia Kassaija wa Uganda, nae alitangaza kwamba nchi yake itatia nguvu kuwekeza katika kilimo na ufugaji na hata, utengenezaji wa mafuta hususani kwenye eneo la Albertini Graben ambako ilivumbuliwa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.