kwamamaza 7

Mfalme wa zamani wa Rwanda Kigeli V Ndahindurwa afariki

0

Mfalme wa zamani wa Rwanda Kigeli V Ndahindurwa amefariki dunia akiwa uhamishoni nchini Marekani. Habari za kifo chake juzi usiku zimethibitishwa na magazeti mbali mbali ijapokuwa familia yake haijatoa taarifa rasmi.

Mfalme huyo alitawala Rwanda kwa miaka miwili tu kwanzia mwaka 1959 hadi 1961 wakati utawala wa kifalme ulipong’olewa kupitia kura ya maamuzi na kumlazimisha kwenda uhamishoni.

Hata hivyo hakuweza kurejea nchini mwake kwa kutofautiana na utawala uliopo sasa nchini Rwanda.

[ad id=”72″]

Leti kigeli V Ndahindurwa alizaliwa tarehe 29 Juni 1936 sehemu ya kamembe magharibi mwa Rwanda, baba yake alikuwa Yuhi Musinga; alikuwa na ndugu 14 akiwa wa mwisho.

Alipokuwa mtoto mwenye umri wa miaka 4, baba yake alihamishwa Moba (Congo) na serikali ya ubelijiji. Baada ya kifo cha baba yake katika jamhuri ya kidemokarasi ya Congo, Kigeli alirudi Rwanda mnamo mwaka wa 1944 na kupewa jina la Jean Baptiste.

Théogène U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.