Home SHERIA Meya wa Rubavu yakamatwa kwa kashfa za kukiuka haki za wagombea
SHERIA - July 22, 2017

Meya wa Rubavu yakamatwa kwa kashfa za kukiuka haki za wagombea

Kulingana na habari kutoka Polisi ya Rwanda ni kwamba meya wa wilaya ya Rubavu amekwisha kamatwa kama mwanzo wa uchunguzi dhidi ya wanaokiuka haki za wagombea urais.

Chapisho hilo la tovuti ya Polisi ya Rwanda linaendelea kusema kwamba viongozi wa ngazi za chini wanaonywa kwamba yeyote atakayethubutu kuvunja utaratibu wa mgombea yeyote atachukuliwa hatua kwa kuwa wagombea wote wana haki sawa.

ACP Theos Badege ambaye ni msemaji wa Polisi ya Rwanda amesema kwamba mpaka sasa kumekwisha asilishwa kesi za madai kama haya nne kwa njia halali ikiwemo kwa upande wa Tume ya Uchaguzi, na hata upande wa wagombea.

Badege anaendelea kusema kwamba uchunguzi juu ya kesi hizo nne umekwisha anza, ikiwemo uchunguzi dhidi ya meya wa Rubavu ambaye amekwisha kamatwa.

 

Inasemekana kuwa kuna viongozi wawili ambao wako kizuizini na chini ya uchunguzi wa polisi akiwemo meya wa Rubavu na hata Katibu mtendaji wa Tarafa ya Busanze ya wilaya ya Nyaruguru.

Ameendelea kusema kwamba kesi nyingine nne zilizoripotiwa kutoka tarafa za Gahara na Rwimiyaga za wilaya ya Nyagatare na hata nyingine kutoka wilaya ya Kirehe zinafanyiwa uchunguzi.

Kuna habari zinazosema kwamba meya wa Rubavu amekamatwa akiwa kwenye Hoteli pamoja na Bi Dukundimana Esperance aambaye ni mfanyakazi wa wilaya anayejadili maswala ya wafanyakazi wa umma.

Inasemekana pia kwamba Ugirirabino Elzaphan, Katibu Mtendaji wa tarafa ya Nyamyumba naye amekamatwa.

Meya wa Rubavu ambaye amekamatwa hakuhudhuria shughuli za kampeni za mgombea wa chama cha RPF zilizofanyika tarehe 20 Julai.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine inasemekana kwamba meya huyo hakumukaribisha mmoja wa wagombea wa urais wa Rwanda ila duru za karibu ya mgombea huyo zimekanusha habari hizo kwa kusema walikwenda hapo wakipeleka barua ambayo ilipokewa bila tatizo.

Habari hizi zinajiri baada ya waziri wa utawala wa ndani na serikali, Françis Kaboneka, kutoa kauli ya kuwaonya viongozi wanaozuia shughuli za wagombea kwamba hatua zitachukuliwa dhidi yao kulingana na masharti ya kura.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.