kwamamaza 7

Meya wa Rubavu aachiliwa huru

0

Ikiwa kumekuwa kukitarajiwa kusikizwa mahakamani kesi ya Sinamenye Jeremie kuhusu kufungwa ama kuachiliwa huru mwishowe habari zilithibitisha kwamba meya huyu anayetuhumiwa kutatiza shughuli za wagombea urais ameachiwa huru.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baada ya watu waliokuja kushiriki kesi iliyokuwa ikitarajiwa kuanza saa tatu, wakiwemo waandishi wa habari na watu wengine kuambiwa na mahakama kwamba watalazimika kungoja hadi hitilafu ya mfumo wa tekniki waliyokutana nayo kukosolewa mawakili wa meya Sinamenye Jeremie walifika mnamo saa nne na kuwaambia kwamba mteja wake ameachiwa huru. Meya huyu alikuwa akikaa gerezani kwa siku nane. Mshatakiwa mwenza Dukundimana  Esperance naye ameachiwa huru ambao wote wanashtakiwa kutatiza shughuli za mgombea urais.

Me Nsengiyumva Straton amesema

“imekuwa ikitarajiwa kusikizwa kesi kuhusu kufungwa ama kuachiliwa huru ila baada ya uendeshaji mashtaka kuona kwamba kwa mjibu wa sheria haiko muhimu, imeamriwa kwamba watakuwa wakiitika mahamani wakiwa huru. Na jingine ni kwamba meya atarudi kazi yake kama kawaida”.

Waandishi wa habari walipotaka kujua sababu ambayo kauli hii inatolewa na mawakili wa mshtakiwa, walimhoji Kayitare Jean Baptiste mwendeshaji mashtaka ya ngazi ya juu ya Rubavu na akawaambia kwamba wana mwendeshaji mashtaka mkuu ambaye angewapa maelezo zaidi.

Walipotaka kuzungumza na mwendeshaji mashtaka mkuu, waandishi wa habari hawakuweza kumpata kwenye simu kwa sababu aliwaambia kwamba yuko mkutanoni.

Mwenyekiti wa mahakama kuu ya Rubavu alipoongea na Bwiza.com kwenye simu alieleza kwamba wakati kuna hitilafu ya kitekniki kesi za dhuraru ikiwemo kama hiyi zinaamriwa kwa njia za kawaida ambapo ndivyo ilivyokuwa kwa hiyi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.