kwamamaza 7

Meddy kutumbuiza Bugesera katika tamasha ya “ Mutzig Beer Fest”

0

Msaani maarufu hapa Rwanda na eneo la Afrika ya Mashariki Ngabo Medard( Meddy) anayefanyia shughuli za muziki wake nchini Umarekani atarajiwa kufika Rwanda ambapo amekuwa hajafika miaka 6 iliyopita.

Meddy arudi Rwanda kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 ambako amekuwa akipanga kuja na shughuli zake zikagongana huku ikamfanya kutokuja.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Msanii huyu alikuwa maarufu kwa nyimbo za mtindo wa pop na R&B na baada ya kuhamia Umarekani alitunga vibao vingine kama Holy Sprit, Nasara, Ntawamusimbura na kadhalika.

Meddy atakuja Rwanda kupitia mwito wa kiwanda cha BRALIRWA kilichoanda tamasha ya Mutzig Beer Fest ambayo inafanyika kila mwaka. Tamasha hiyo itafanyika Bugesera mjini Nyamata tarehe 02 Septemba 2017 katika bustani ya Golden Tulip Hotel Hotel.

Meddy ameiambia tovuti ya igihe.com kwamba mpango wa ziara yake nchi Rwanda haujatekelezwa barabara na kwamba hana mengi ya kusema kuhusu mpango huo.

Ingawa imekwisha julikana kwamba Meddy atatumbuiza kwenye tamasha ya Mutzig Beer Fest hawajatambulika wasanii ambao watamshirikisha katika tamasha hiyo.

BRALIRWA imekuwa ikifanya kazi nzito ya kuwaalika wasanii maarufu duniani na hapa barani Afrika kuja kutumbuiza Rwanda kwenye tamasha zinazolenga hususani kufanyia matangazo vinyaji vyake.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.