kwamamaza 7

Meddy afunguka kuhusu wimbo wake –Ntawamusimbura na mpango wake kuja Rwanda

0

Kumekuwa na tetesi nyingi kwamba Meddy huwa anaiga nyimbo za wasanii maarufu na hii imezuka hivi karibuni baada ya kuzindua wimbo wake Ntawamusimbura. Meddy aliurizwa sababau wimbo wake ulifika mbali kulingana na nyimbo nyingine za awali ikiwa haina uhusiano na vile watu wanavyosema.

Meddy ameiambia Bwiza.com kwamba watu huwa wanachanganya mambo hususani kwa kutoelewa mtindo wa mziki wa blues ambao wimbo wake umebuniwa.

“baada ya kutunga wimbo ule-Ntawamusimbura na kuona maneno yaliyoandikwa nilihisi kwamba ingekuwa bora nikuuweka kwenye mtindo wa blues, blues ni mtindo wa zamani na maneno yaliyoandikwa si ya kisasa” Meddy alisema

[xyz-ihs snippet=”google”]

Aliendelea kusema kuwa mziki wa blues una mtindo wa aina yake na huwa ni sambamba hivyo kufanya watu kutotofautisha nyimbo.

Nyimbo ambazo watu walisema Meddy alitunga kibandia ni ule wa Woman Loves wa Robert Kelly, Earned it wa The Weekend na nyinginezo Meddy amesema kwamba kwa kuwa ziko mtindo wa blues zote ndio ikawafanya watu kusema ameiga.

Meddy alijibu pia kuhusu mpango wake wakuja Rwanda na kusema kwamba juhudi zinaendelea ila tu hajafahamu tarehe kamili. Alisema kuwa kuna kundi la watu wanaoajibika na maandalizi ya safari hiyo na wangali bado kwenye mazungumzo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.