kwamamaza 7

Masharti ya kura yaliyoleta mzozo yafutwa

0

Tume ya Uchaguzi imekwisha zindua kanuni ambazo zitafuatwa katika uchaguzi wa rais, kanuni hizi zinafafanua na kuondosha mashaka juu ya uendeshaji kampeni kwa kutumia njia za kiteknolojia.

Kanuni hizi ambazo zilitiwa sahihi tarehe 31 Mei 2017, na Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Prof. Kalisa Mbanda, zimechapishwa katika mtandao wa Ofisi ya Waziri mkuu.

Kanuni hizi zinabeba kichwa “ Kanuni no 02/2017 ya 31/05/2017 zinazobatilisha na kujaza kanuni no 01/2017 za 04/05/2017 za tume la Uchaguzi zinazohusu Uchaguzi wa rais wa 2017.

Kikao cha Makamishna kimeidhinisha kanuni hizi baada ya kurejea kanuni zilizokuwepo No 01/2017 ya 04/04/2017 za Tume ya Uchaguzi mwaka wa 2017, katika ibara zake : la 23, la 28, la 32, la 37, na 38 la 40 na la 41, la 42, la 43, 44 baada ya kufanyiwa uchumbuzi na kuyahalalisha

Mjawapo wa yaliyomo ni kwamba kusaka saini za waungamkono wa mgombea binafsi ,inafanywa siku 30, kabla ya kupokea ugombea na hii ikafanywa kwa kufuata hati inayotolewa na Tume ya Uchaguzi.

Mgombea binafsi ambaye anaomba saini za waungamkono akiwa katika sehemu au taraafa yoyote, anaarifu kwanza madaraka ya wilaya na anatoa nakala kwa Afisa mtendaji wa Tume la Uchaguzi katika eneo ambapo Wilaya hiyo inahesabiwa.

Mgombea binafsi anaweza kuwaomba saini waungamkono wake pekee ama kupitia kwa wakilishi aliyewachagua pekee Lakini wenye umri wa kupiga kura. Orodha ya watakayemsaidia katika utaratibu huu inaasilishwa kwa Tume Kuu la Uchaguzi , siku 15 kabla ya kuanza kuwapigisha saini waunga mkuno.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ni marufuku kubandika vyombo vya kampeni kwenye shule.

Ibara mpya la 5 linasema kwamba wagombea wanaruhusiwa kubandika picha zao na karatasi kwa ajili ya kampeni kwenye majengo ya serikali yaliyoekwa na madaraka ya Wilaya ama tarafa.

Vibandiko hivi kwa ajili ya kampeni vinaweza vikawekwa pia kwenye magari kulingana na maelewano ya pamoja.

Hata hivyo ni marufuku, kueka vyapa kwa ajili ya kampeni kwenye vituo vya afya, shule, makanisa . Wagombea wanahimizwa kutoa wito kwa waunga mkono wake kutochana, kutoharibu na kutofuta picha ya mgombea mwenza, na kuheshimu vyombo vingine kwa ajili ya kampeni.

Kutotumia mali ya uma na kutomdhalilisha mgombea mwenza

Ibara la 6 lililofutwa na kujazwa linaonyesha kwamba ni marufuku kutumia mali ya uma kwa namna yoyote kwa ajili ya kampeni za uchaguzi, popote ambapo mali fulani ilipo tofauti na sheria , kumtukana ama kumdhalilisha mgombea mwenza kwa namna yoyote, kutoa zawadi, ama kupokea na kutoa rushwa, kutenda kwa kuzingatia kabila ama uhusiano wa familia ama ubaguzi wa kidini au kabila.

Kumekuwa marekebisho pia kwenye uendeshaji kampeni wa njia za teknolojia

Kuhusu uendeshaji kampeni kwa kutumia teknlojia, kumekuwa na masharti ambayo yalikuwa yanasema kwamba ujumbe wa mgombea unayetumia njia za teknlojia .anapaswa kupelekwa kwanza kwenye Tume ya Uchaguzi masaa 48 kabla ya kutumiwa ili tume hiyo ikague kwamba usingeleta mzozo.

Hii inajiri baada ya muda si mrefu Kanuni hizi kupingwa na viongozi mbali mbali ikiwemo serikali ya Rwanda na hata mabalozi wa nchi za kigeni waliokuwa wakidai kwamba zinawanyima wagombea uhuru wa maoni

Kanuni hizi zilifanyiwa marekebisho hususani katikaka sharti 38 la Kanuni za tarehe 04/04/2017. Na sharti la sasa linasema inaruhusiwa kuendesha kampeni kwa kutumia tovuti za kijamii , bali ni marufuku kuendesha kampeni kwa kutumia kurasa na tovuti za kijamii za serikali na mengineyo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.