kwamamaza 7

Mashariki mwa Rwanda:  Wanawake wabakwa na mwenye virusi vya ukimwi juu ya kujilipiza kisasi

0

Wanawake Wilayani Bugesera wametangaza kuwa wanabakwa na mume anayejificha msituni Gako na kuwabaka wanaopita eneo hilo.

Imeripotiwa kwamba huyo anaitwa Eric na anafanya hilo kwa kujilipiza kisasi kwa kusema aliambukizwa na mwanamke.

Mwanamke aliyebakwa amesema “ Tulikuwa wanawake wanne tukitafuta kuni. Tulipomuona tulikimbia lakini mimi mti ukanizuia. Alinibaka kwa kutumia vidole na kuniambia anaweza hata kunitoa utumbo. “

“Alipomaliza alimbaka pia msichana aliyekuwa karibu.” Ameongeza

Kiongozi wa Wilaya ya Bugezera,  Richard Mutabazi amesema ulinzi umetiliwa mkazo ili kumkamata Eric na kuwaonya raia wasikanyage katika msitu wa Gako.

Kuna taarifa kwamba Eric aliwahi kufungwa kwa kumbaka mwanamke kisha akaachiwa huru.

Wananchi wameitaka serikali kumkata ili walionyanyaswa wapate haki.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.