kwamamaza 7

Maseneta wa Marekani waitaka Rwanda kumuachia huru mwanasiasa Diane Rwigara

0

Makamu Kiongozi wa maseneta  (Democrate), Dick Durban ameitaka serikali ya Rwanda kumuachia huru  mwanasiasa Diane Rwigara na mama mzazi wake, Adeline Rwigara.

Seneta Durban amesema Rwanda haistahili kumfanya asimame kizimbani Diane Rwigara kwa kuwa anayoshtakiwa hayaeleweki.

Kupitia ukuta wake wa twitter, Durban ameandika “ Nina wasiwasi kutokana na uhalifu anaoshtakiwa Diane Rwigara ambao haueleweki.”

Huyu ametangaza inawezekana kwamba Diane Rwigara anashtakiwa kutokana na kitendo cha kutaka kuwania ugombea wa urais mwaka 2017.

“ Kiukweli inaonekana kwamba haya yote ni kutokana na kutaka kuwania ugombea wa urais.”

Mwingine ambaye ni Seneta wa Missouri, Agnes Wagner ameitaka Rwanda kumuachia huru Diane Rwigara kwani hana kosa lolote.

“  Leo tunaitaka Rwanda kumuachia huru Diane Rwigara kwani kufanya mambo ya kisiasa kwa amani si kosa.”

Akizungumza kuhusu kisa cha Diane Rwigara kufungwa gerezani, Rais Kagame alipokuwa nchini Ufaransa tarehe 11 Novemba 2018, alisema Diane Rwigara hakufungwa kwa ajili ya haja yake ya kuwania kuwa mgombea wa urais.

“ Anashtakiwa kuunda  orodha bandia ya watu wanaomfuata ili ugombea wake uwe sahihi. Alilofanya si kwamba ni kinyume na sheria lakini linazuwa matatizo mengi.” Rais Kagame alisema.

Diane Rwigara anashtakiwa kutumia hati bandia wakati wa kuwania ugombea wa urais, kuzua ghasia nchini pamoja na mama yake anayeshtakiwa ubaguzi.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.