Swahili
Home » Maseneta wa bunge la Rwanda waweka wazi Ofisi za Ubalozi za Rwanda zimezeeka
HABARI SIASA

Maseneta wa bunge la Rwanda waweka wazi Ofisi za Ubalozi za Rwanda zimezeeka

Bunge la Rwanda, baraza la seneti,wanaojumuika kwenye kamati ya mambo ya nje laomba Ofisi za Balozi za Rwanda kukosolewa ama kuhamishwa ili ziweze kurahisihisha utekelezaji kazi.

Kuna baadhi ya majengo ya balozi anayoonekana kuwa amezeeka mno, mojawapo ni jengo la ubalozi wa Rwanda la Washington DC na hata la New York. Majengo haya yamekwisha zeeka kama ilivyobainishwa kwenye ripoti hii iiyoasilishwa na kamati ya seneti mambo ya nje ambapo wanaagiza kujengwa kwa majengo mapya.

Rwanda ina mpaka sasa majengo ya balozi yapatayo 33 ambayo huendeshwa shughuli za kibalozi za nchi zipatazo 147, za eneo hili, nje yake na mashirika ya kimataifa na hata ofisi za balozi ndogo 37 zinazotetea maslahi ya Rwanda kwenye nchi za kigeni zipatazo 17 kama ilivyotangazwa na KT Press.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Maseneta wa Rwanda wamegusia pia kuongezeka kwa Balozi za Rwanda katika nchi nyingine kusikokwenda sambamba na kuongezeka kwa mabalozi wa kifundi wanaofaa kutekeleza wajibu wa ubalozi. Kama suluhu kwa tatizo hili, maseneta wamesema kungeajiriwa mabalozi wa kujizoeza ambao wangefanya kazi kwa kuiga wale wa kifundi ili waje wakapata uzoefu utakaowawezesha kufanya kazi yao ipasavyo. Seneta Michel Rugema asema “ inachukuwa muda mlefu kumfundisha balozi wa kifundi”

Dkt. Richard Sezibera aliyekuwa katibu mkuu wa EAC naye ni mmoja mwa wale wanaounda kamati ya mambo ya nje.

Miongoni mwa yale waliyoagiza ni kutafuta jinsi ya kuwarahisisha watoto wa mabalozi kufuata masomo yao. Hapa kulitolewa wazo la kwamba mabalozi wangelipia karo watoto wao badala ya serikali. Dkt. Sezibera asema kungefikiriwa jinsi ya vile mabalozi wangelipia watoto wao karo na hivyo bila kuathiri bajeti wanatolewa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com