kwamamaza 7

Marubani walifanya lolote kuidhibiti ndege aliyokuwemo Mnyarwanda-Ripoti mpya

0

Ripoti ya uchunguzi kuhusu kuanguka kwa ndege ya Ethiopia Airlines mwezi uliopita inasema kuwa ndege hiyo ilitaka kuangukia pua yake mara kadhaa kabla ya ajali hiyo.

Marubani walifuata maagizo yaliopendekezwa na Boeing kabla ya ajali hiyo kulingana na ripoti ya kwanza ya ajali hiyo.

”Licha ya juhudi zao , marubani walishindwa kuidhibiti ndege hiyo” , alisema waziri wa uchukuzi Dagmawit Moges.

Ndege hiyo aina ya ET302 ilianguka baada ya kupaa kutoka mji wa Adis Ababa,na hivyobasi kuwaua watu 157. Moja wao alikuwa Mnyarwanda, Musoni Jackson ambaye alikuwa akienda kuhudhuria mkutano nchini Kenya.

Ilikuwa ndege ya pili aina ya Boeing 737 kuanguka katika kipindi cha miezi mitano.

Mwezi Oktoba mwaka uliopita , ndege aina ya Lion Airflight JT610 ilianguka baharini karibu na Indonesia na kuwaua watu wote waliokuwa wameabiri.

”Wafanyikazi wa ndege hiyo walijaribu kila mbinu walizoelezewa na mtengenezaji wa ndege hiyo lakini walishindwa kuidhibiti” , bi Moges alisema katika mkutano na wanahabari mjini Adis Ababa.

Katika taarifa , afisa mkuu wa Ethiopia Airlines , Tewolde GebreMariam alisema kuwa alifurahishwa na kazi ya marubani hao kujaribu kuidhibiti ndege hiyo.

”Ni bahati mbaya kwamba walishindwa kuidhibiti ndege hiyo kutoangukia pua yake”, ilisema kampuni hiyo ya ndege katika taarifa yake.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.