kwamamaza 7

Marekani:Gari linalojiendesha lahusika na ajali mjini Las Vegas

0

Gari hilo lililokuwa limewabeba abiria kadha liligongwa na lori lililkuwa katika mwendo wa chini.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa ajali hiyo ambayo maafisa wanaema ilitokana na hitilafu ya dereva wa lori.

Basi hilo ndilo la kwanza la aina yake kutumiwa kwenye barabara za umma.

Ajali hiyo ilitokea siku moja baada ya Waymo – inayomilikiwa na kampuni ya Google, Alphabet, kutangaza kuwa inazindua teksi zinazojiendesha huko Phoenix, Arizona.

Basi hilo linawabeba hadi wau 15 na lina kasi ya hadi kilomita 45 kwa saa lakini kawaida mwendo wake ni kilomita 25 kwa saa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Msemaji wa mji wa Las Vegas aliiambia BBC kuwa ajali hiyo ilkuwa ni kidogo na kwamba basi hilo litarudi barabarani Alhamisi baada ya majaribio ya kawaida.

Lori la mizigo lilikuwa likitoka kupakia mizigo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Basi likafanya kile linastahili kufanya na kusimama. Kwa bahati mbaya dereva wa lori hakusimama, alisema afisa wa mawasiliano Jace Radke.

Ajali za magari yanayojiendesha zimeripotwa awali, lakini karibu ajali hizo zote zimesababishwa na makosa ya wanadamu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.