kwamamaza 7

Marekani: Ibada ya kumuaga mfalme wa Rwanda Kigeli V Ndahindurwa

0

Tangazo la wanafamilia wa leti mfalme wa mwisho wa Rwanda Kigeli Ndahindurwa John Baptist lililotiwa saini na mshauri wa zamani wa Kigeli, Boniface Benzige, linatoa mwito wa kumuaga leti mfalme na kuunga mkono familia katika ibada yake ya mwisho leo.

Ibada ya mwisho ya kumuaga kigeli V Ndahindurwa inategemewa saa tano na nusu leo tarehe 31 Oktoba 2016 katika kanisa la St Athanasius Church.

Mfalme aliyefariki tarehe 16 Oktoba 2016 katika hospitali ya Fairfax huko Marekani, mazishi yake yalizaa utata kama angezikwa Marekani au katika nchi ya kizazi yaani Rwanda.

[ad id=”72″]

Soma: Utata juu ya mazishi ya mfalme wa mwisho wa Rwanda

Wiki iliyopita, kundi la wanafamilia pamoja na Ezra Mpyisi aliyekuwa mhudumu wa mfalme walifika Marekani kuzungumza kibinafsi na wanafamilia wanaoishi nchini humu juu ya mahali pa kufanyia mazishi; hadi sasa hivi mahali pa mazishi yake hapajatangazwa bado.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.