kwamamaza 7

Marais Kumi wenye mshahara mkubwa Afrika

0

Marais wa nchi za Afrika huwa wanalipwa mshahara unaooneka kuwa mkubwa kulingana na uwezo wa nchi zao. Jambo hili linaweza kulinganishwa na tabia ya viongozi wa Afrika wa kupora na kumiliki mali ya umma.

Jacob Zuma ambaye ni rais wa Afrika Kusini ndiye anayeongoza orodha hii akiwa na mshahara mnono wa dola elfu 272,000.Nchi ya Afrika Kusini pia ndiyo nchi yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi barani hili. Marais wa nchi za Afrika ya mashariki wanaokuja kwenye orodha hii ni pamoja na Uhuru Kenyatta wa Kenya anayeshika nafasi ya tatu mtawalia na mshahara wa 132,000$ na rais Kagame Paul wa Rwanda anayeshika nafasi ya 10 na mshahara wa 85,000$

[xyz-ihs snippet=”google”]

10.Paul Kagame (Rwanda) – 85,000$

Paul Kagame, ni rais tangu 2000 mwaka akimrithi Pasteur Bizimungu aliyejiuzuru, wakati ambapo Kagame amekuwa rais wa muda hadi 2003 alipochaguliwa na wanyarwanda.

9.Ellen Johnson Sirleaf (Liberia) – 90,000$

Ellen Johnson ni rais wa kike wa kwanza kuitawala nchi ya Afrika tangu mwaka 2006. Amekuwa ni rais wa 24 kuitawala Liberia.

8.Alassane Dramane Ouattara (Côte d’Ivoire) – 100,000$

Perezida Ouattara aliitawala Kodivaa tangu mwaka wa 2011 akimrithi Laurent Bagbo ambaye anafuatia kisheria.

7.Ali Zeidan (Libya) – 105,000$

Alikuwa rais tangu mwaka 2012 hadi mwaka 2014 kabla yakuondoshwa madarakani na kamati ya bunge mwaka tarehe 14 Machi 2014 na kuihama nchi wakati huo alikuwa ndiye rais wa 7 anayelipwa mshahara mnono barani Afrika.

6.Denis Sassou Nguesso (Congo) – 110,000$

Denis Sassou Nguesso ni rais wa Kongo tangu mwaka wa 1979 hadi 1992 hapo aliondoka madarakani na kushika kiti cha urais tena toka mwaka wa 1997 hadi wakati huu. Alipata pia mafunzo ya juu ya Kijeshi toka nchi za nje.

5.Hage Geingoba (Namibia) – 110,000$

Rais huyu ambaye anaitawala nchi tangu mwaka wa 2015 ana pia shahada ya uzamivu(PHD) kutuko chuo cha Uingereza cha Leeds.

4.Azali Assoumani (Comoros) – 115,000$

Azali Assoumani ni rais wa nchi hii ambayo iko miongoni nchi ndogo za Afrika na alishika utawala baada ya kuangushwa kwa utawala wa Tadjidine Ben Said Massounde.

3.Uhuru Kenyatta (Kenya) – 132,000$

Uhuru Kenyatta ni rais wa 4 wa Kenya ambaye anatawala nchi hii inayosifika kuwa na uchumi imara kwenye Afrika ya Mashariki.

2.Abdelaziz Boutefrika (Algeria) – 168,000$

Abdelaziz Boutefrika ni rais tangu mwaka wa 1999. Alizaliwa Moroko na baadaye akaja kuitawala nchi ya asili yenye hazina kubwa ya mafuta mwaka wa 1999.

1.Jabob Zuma (Afurika y’Epfo) – 272,000$

Rais Zuma Alichaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini mwaka wa 2009. Rais huu pia anatawala kwa nafasi ya nne kwa orodha ya marais wanaolipwa mshahara mnono duniani.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.