kwamamaza 7

Mali asili ya Burundi huibiwa kupitia Rwanda na DR Congo- Rais Nkurunziza

0

Rais wa Burundi  Pierre Nkurunziza amesema mali asili ya Burundi kama vile Kahawa na madini huibiwa kupitia Rwanda na DR Congo.

Rais Nkurunziza amesema  haya jumatatau wiki hii katika hotuba yake ya kuanzisha uchimbaji wa madini wilayani  Butihinda, mkoa wa Muyinga.

Kwa hayo, Rais Nkurunziza amewahamasisha wakazi karibu na mpaka wa Rwanda na DR Congo kuwa tahadhari kwa kupambana na huu wizi.

Kwa mujibu wa taarifa za RTNB, Nkurunziza amesema migodi ya nchi ni nema ya Mungu na kuwataka Warundi wailinde mali yao wenye wivu.

Pia Rais Nkurunziza amewataka Warundi kuekeza mali yao kwa kuwa kuna usalama nchini humo kama ilivyofanya .Afircan Mining Burundi

Mala nyingi Warundi walikamatwa nchini Rwanda wakiuza madini na kahawa kutoka Burundi kinyume na sheria

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.