kwamamaza 7

Malawi yaanzisha uchunguzi kwa wanyarwanda 36 juu ya mauaji ya kimbari

0

Serikali ya Malawi imeanza upelelezi kwa wanyarwanda wanaoishi pale ambao waliwekwa kwenye orodha ya watoro wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yalipatikana mnamo 1994.

Rwanda imeomba nchi ya Malawi kuwakamata watuhumiwa 36 wa mauaji ya kimbari na kuwahamisha nchini Rwanda ili kuwekwa mahakamani na kutoa maelezo kuhusu mchango wao katika mauaji yalisababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja.

Katibu mkuu katika wizara ya mambo ya ndani, Beston Chisamile ameambia CAPITAL FM kwamba serikali imeanza upelelezi kwa wanyarwanda wanaotuhumiwa ili kujua idadi yao.

Mtuhumiwwa Vincent Murekezi ametiwa mbaroni
Mtuhumiwwa Vincent Murekezi ametiwa mbaroni

Alisema, “Sina habari kamili kuhusu tukio hili lakini tulichofanya kuhusu ombi hilo ni kuanzisha uchunguzi, ndiyo itakuwa rahisi kutoa maoni zaidi.” Aliongeza kwamba serikali haijapata maandishi rasmi ya kuomba uhamishaji wa watuhumiwa hao.

Mtuhumiwa mwingine, Vincent Murekezi alikamatwa na shirika za usalama nchini Malawi mnamo 8 Disemba 2016 baada ya kushinda siku kadhaa akiwa huru. Mfanayabiashara huyu alikamatwa ya kubadilisha pasipoti yake.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.