kwamamaza 7

Malawi: Vikwazo vimetolewa ili Murekezi arejeshwe Rwanda

0

Rwanda na Malawi wametia saini kwa mkataba ya kuwa wanapatiana wakosefu, mkataba ulio kua kikwazo ili kumurejesha raia wa Rwanda, Vincent Murekezi anaye tafutishwa na mahakama ya Rwanda, wakati yeye ameishi Malawi muda murefu.

Siku nenda ndipo mwendesha mashtaka wa mahakama ya Lilongwe aliamua kutorejesha Murekezi Rwanda kwa sababu hapakuwepo mkataba wa kuwasiliana kati nchi mbili kwa ajili ya wakosefu wanao kimbia nchi yao na kwenda nchi nyingine.

Kamati ya haki za binadamu HRCC, inashukuru mkataba huo, wakati huo ilishutumu uongozi wa mahakama na wizara ya sheria hata mtume maalum wa serikali kwa kuwa walishindwa kushauria polisi ili kutatua swala hilo hata kama Murekezi ni mfanya biashara wa hali ya juu na alisaidia kwa ngambo ya uchumi akipana kodi, kuweka mtu kama huo anaye shutumiwa mauaji ya Kimbari inalinganishwa na kuzarau wakaaji wa Rwanda.

HRCC inasema kuweka Murekezi na wengine kama yeye ambao hutafutiwa na sheria ya Rwanda, ni kusema wanawapenda wakosefu na ni ujumbe kimataifa ya kuwa Malawi inaweka wakosefu kama vile husema kiongozi wa HRCC, Robert Mkwezalamba.

Sherehe ya kusaini mkataba ulifanyika katika wizara ya uhusiano na mataifa mjini Lilongwe, Malawi ikisimamiwa na waziri wa uhusiano wa kimataifa Francis Kasasila akiwa pamoja na waziri wa sheria Samuel Tembenu, kwa upande wa Rwanda palikuwepo waziri wa sheria Johnston Busingye.

Nchi ya Malawi husemwa ya kuwa huwaweka raia wa Rwanda karibu 5.000, 36 kati yao ikifikiriwa kuhusika na mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi, wamoja wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Dzaleka na wengine wengi wakiwa wafanya biashara pamoja na wakaaji wa Malawi.

Polisi ya Malawi ilitia mbaroni Vincent Murekezi tarehe 8 Disemba 2016 baada ya kundi Concerned Citizens lilitia mkazo na kusema raia huo wa Rwanda akamatwe kwa sababu anashutumiwa kuhusika na mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi nchini Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.