kwamamaza 7

Majina ya ‘waliosajili’ Wanyarwanda 43 waliokamatwa nchini Uganda yatiwa hadharani

0

Majina ya watu watano ambayo yanasikika kama ya Wanyarwanda  yamejitokeza kwenye orodha ya watu ‘walioshiriki’ katika mambo ya ‘kusajili’ Wanyarwanda 43, ambao walikamatwa wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Tanzania na Uganda,Kikagati kwa kutumia hati zinasomekana kuwa ‘bandia’.

Taarifa za  chombo cha habari nchini Uganda Virunga post zimeeleza kwamba bilashaka walioshiriki katika kitendo hiki  ni Dk.Ruvumwa aliyewahi kutekwa nyara kisha akaachiwa huru,Geoffrey Musoni ambaye aliwahi kuwa mwanajeshi wa Rwanda(RDF),ambaye ni mkazi wilayani Mukono,Moses Bijura ambaye ni mkazi wilayani Ntungamo,Charles Sande maarufu kama Robert Mugisha na mwingine kwa jina la Felix Mwizerwa.

Taarifa hizi zinaendelea kusema kwamba hawa wanaendelea kusajili watu wengine wa kujiunga na jeshi la  RNC nchini DR Congo eneo la Minembwe kwa msaada wa maafisa wa upelelezi wa Uganda,CMI.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,lengo la safari ya Wanyarwanda hawa lilizusha mkanganyiko kwa kuwa baadhi ya vyombo vya habari vilisema kwamba hawa walikuwa wakielekea nchini Burundi katika shughuli za kidini taarifa ambazo ni tofauti ni nyingine zilizoenea kwamba hawa walikuwa wamesajiliwa kujiunga na jeshi la RNC la jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa ‘linalodhamiria’ kuishambulia Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.