kwamamaza 7

Majina mazito yanayojitokeza katika visa vya Wanyarwanda nchini Uganda

0

Baada ya visa vilivyozagaa kwamba Wanyarwanda wanakamatwa na kuteswa kimwili na maafisa wa upelelezi wa Uganda,CMI kwa mashtaka ya kuwa wapelelezi wa Rwanda,kuna watu watau wenye majina mazito nchini Uganda waliojitokeza kwa sasa katika visa hivi.

Miongoni mwa hawa kuna kiongozi wa ofisi ya upelelezi nchini Uganda,Brig.Jenerali Abel Kandiho.Huyu anatajwa  mala nyingi na vyombo vya habari nchini Uganda hasa Virunga post kuwa anawasaidia wanachama wa RNC kuendelea na shughuli zao za kusajili vijana asili ya Rwanda kutoka kambi za wakimbizi nchini Uganda ili kujiunga na jeshi la Jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa nchni DR Congo.

Mwingine ni waziri wa usalama  wa ndani,(Rtd) Luteni Jenerali Henry Tumukunde ambaye alikosolewa na vyombo vya habari hasa The Standard nchini Kenya kwamba kuhusu kisa cha Wanyarwanda waliokuwa wakitoa ombi bungeni kuhusu usalama wao.Kuna taarifa kwamba huyu ni rafiki wa dhati wa Jenerali Kayumba Nyamwasa na kuwa mala nyingine anamtembelea nchini Afrika kusini kama ilivyotangazwa na Chimpreports.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia kuna mwanamke Sarah Kagingo ambaye aliwahi kuwa mfanyakazi ikuluni.Huyu ni mwenyeji wa chombo cha habari Soft powe.com,kwa mujibu wa taarifa za Virunga post,chombo hiki kinatangaza uongo kuhusu visa vya Wanyarwanda nchini Uganda kwa kuegamia upande wa RNC.

Taarifa hizi zinasema kwamba Sarah Kagingo anashirikiana mno na ami ya Rais Museveni,Jenerali Caleb Akandwanaho maaruku kama Salem Saleh.

Kwa ujumla,serikali ya Uganda ilielezea  Rwanda kuwa Wanyarwanda  wanaokamatwa nchini Uganda ni wale ambao wanahuisiana na vitendo vya ugaidi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.