kwamamaza 7

Maisha ya Ingabire Victoire Umuhoza yangali katika hali mbaya-Mwanasheria wake afunguka

0

Mwanasheria wa Ingabire Umuhoza Victoire kwa jina la Me Catherine Buisman  kupitia barua aliyoandikia Wizara ya Haki ya Rwanda alieleza  anahitaji  kujua kwa nini mteja wake anafungwa katika hali mbaya  baada ya kutoa ombi la kupatiwa haki yake,RFI imetangaza.

RFI imeeleza kwamba Me Buisman alisema baada ya hili ombi Ingabire Victoire alifungwa katika hali mbaya kama vile kukataliwa kukutana na familia yake, kutotembelewa na wanachama wake FDU-Inkingi.

Huyu Mwanasheria amefafanua Rwanda ilikaa kimya na haikufanya lolote kuhusu kumpa haki kama ilivyoamua mahakama ya kutetea haki za binadamu barani Afrika.

Kwa upande wa Rwanda, Waziri Makamu kwenye Wizara ya mambo ya nje Olivier Nduhungirehe amesema Rwanda haitatii uamuzi wa hii mahakama kwani inafanya kazi zake kwa ajili za kisiasa.

“Tulieleza vizuri kuwa Rwanda haitakubalia hii mahakama kuwa kifa cha kujaribu kubadili uamuzi wa mahakama za ndani ” Olivier alisema

“Tunajua kwamba kesi hii ilihukumiwa na mahakama ya juu nchini kumfunga Ingabire Victoire miaka 15” aliongeza

Mahakama ya kutetea haki  barani Afrika iliyoko Nchini Tanzania mjini Arusha miezi sita iliyopita iliomba serikali ya Rwanda kumpa haki zake Ingabire Victoire kama vile uhuru wa kujieleza na kupata mwanasheria.

Ingabire Umuhoza Victoire alihukumiwa kufungwa miaka 15 juu ya uhalifu wa kupuuza mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.