kwamamaza 7

Mahali kiongozi wa M23 Gen. Sultani Makenga yupo pamejulikana

0

Baada ya siku nenda taarifa ilisema ya kuwa wapiganajei wa M23 pamoja na kiongozi wao hakuna anaye fahamu mahali walipo, ila kwa sasa husemwa ya kuwa yawezekana kujua mahali walipo.

Mwezi nenda jeshi la Uganda lilisema ya kwamba Makenga hayupo tena kambini, na baada ya hapo wapiganaji wengine wakatoroka kambi Uganda na waliendelea na kusema ya kuwa hawajui mahali walipo.

Erique Gasana, mpiganaji wa M23 alikamatwa na jeshi la Congo FARDC, alisema ya kuwa Makenga na kundi la jeshi lake wapo katika wilaya ya Rutchuru jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Eti”nilikuwa pamoja na wanajeshi wengine wa Makenga, tulipanda gari wakitudanganya kuwa tunakwenda kujiunga na jeshi la nchi, tulivuka mpaka tukajikuta tupo tena katika misitu”, hapo na ndipo aliamua kutoroka na kuwaacha wakipanga kushambulia walinzi wa wanyama ili kuwanyanganya silaha na kushambulia sehemu ya Bukina kama vile husema radio Okapi.

Aliendelea na kusema ya kuwa hilo jeshi la M23 liliongozwa na Colonel Joseph Mboneza . Gen. Makenge yupo pamoja na sokomutu katika milima mirefu ya Sarambwe, wilaya ya Rutchuru kando ya mlima wa Sabyinyo na Mikeno karibu na mpaka wa Uganda. Yawezekana Makenga akiwa pamoja na wana jeshi zaidi ya 100 walio toroka kambi la Bihanga, nchi ya Uganda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa hio imehakikishwa na wanao husika na haki za biandamu CEPADHO kwa kuwa wapiganaji hao wapo katika misitu ya Congo.

CEPADHO imeomba serikali ya Congo kuongeza kuwasiliana na kimataifa ili kupambana na wapiganaji wa M23 kwa ajili ya kutafuta amani.

Kundi la M23, ni moja ya makundi yalio semwa muda murefu katika misitu ya Congo, na waliweza kukaba sehemu tofauti katika Kivu ya Kaskazini miaka ya 2012-2013.

Siku zilizo pita wapiganaji hao walipambana na jeshi la Congo, wakashambuliwa wamoja wakakimbilia Rwanda na wengine Uganda, hivi wanajikusanya tena.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.