kwamamaza 7

Mahakama ya Uingireza yakataa kukabidhi kesi za wanyarwanda tano kwa mahakama za Rwanda

0

Kesi za wanyarwanda tano ambao wanashtakiwa kuhusika na uhalifu katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi wa 1994 hazitaendeshwa na Mahakama za Rwanda.

Hii ni baada ya mahakama ya Uingireza  kukataa kukabidhi kesi zao kwa mahakama za Rwanda kwa madai kwamba wangenyimwa haki na mahakama za Rwanda na kukatia kesi za kuegama.

Wanyarwanda hao wote ni pamoja na Vincent ‘Brown’ Bajinya, Charles Munyaneza, Emmanuel Nteziryayo, Celestin Ugirashebuja na Celestin Mutabaruka.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Washtakiwa hawa wote walifanya uhalifu wakiwa kwenye nyadhifa mbalimbali katika utawala wa aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana

Dkt. Vincent Bajinya alikuwa mwandani wa rais Juvenal Habyarimana na alikuwa mwanachama wa MRND kabla ya chama cha CDR kuundwa mwaka wa 1993. Anashtakiwa kuhamasisha watu wa kabila la kihutu kujitenga na watutsi. Anashtakiwa pia kuhusika na mauaji ya watu.

Charles Munyaneza yeye alikuwa diwani wa wilaya ya Kinyamakara katika mkoa wa Gikongoro. Mashtaka dhidi yake ni pamoja na kuhamasisha wahutu kuwaua watutsi, kuandaa mikutano ya kwa ajili ya mauaji, kupora na kuharibu mali za watu, na hata kuwaadhibu watu ambao walikuwa wanapora mali za watutsi bila kuwaua. Anashtakiwa pia kuongoza shambulizi lililowaua watutsi wengi sana katika Ruhashya karibu na mto Mwogo.

Emmanuel Nteziryayo alikuwa meya wa wilaya ya Mudasomwa katika Gikongoro. Anashtakiwa kufanya mikuno na madiwani na hata kuwapa silaha. Huyu pia alikuwemo katika mkutano pamoja na Charles Munyaneza uliowakuatanisha madiwani wakitoa ripoti ya watutsi waliokwishauawa katika kila tarafa wanazoongoza.

Celestin Ugirashebuja naye alikuwa meya wa wilaya ya Kigoma na mwanachama wa MRND,huyu aliitisha mikutano na madiwani ya kuwahamasisha kuwaua watutsi. Alitoa pia masharti ya kuwaua watutsi.

Celestin Mutabaruka yeye alikuwa mkurugenzi wa kituo cha misitu cha Crete-Congo Nil na hapo ndipo alianza vitendo vyake vya kuwatesa watutsi na hata kubagua.

 

Baada ya maamuzi ya kaimu Jaji mkuu wa wilaya, Albhuthnot ya mwaka 2015 ya kutoacha kesi za watu hawa kuendeshwa Rwanda  na Uendeshaji mashtaka wa Rwanda kukata rufaa mahamakama imeamua vilevile kutowaacha na kesi  za wanyarwanda hao kuendeshwa na mahakama za Rwanda.

 Mahakama hiyo ilidai kwamba uamuzi wa kuwapeleka kusikiza kesi zao nchi Rwanda ungetokea kuwanyima haki ya kutopewa haki sawa mahakamani. Na kwa hivyo ingekuwa kinyume na kifungu 6 cha kanuni za haki za kibinadamu na hata waya ya 87 ya kanuni za 2003 ya kupashana wahalifu.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.