kwamamaza 7

Mahakama uhispania kuamua fedha mbadala ya kifungo cha miezi 21 ambazo Lionel Messi atalipa

0

Inasubiriwa ikiwa Lionel Messi atalipa kitita cha fedha kwa ajili ya kukwepa kifungo cha miezi 21 ambacho alihukumiwa na mahakama ya Uhispania kwa kosa la kulagai kodi.

Baada ya Mahakama ya kutoa uamuzi wake wa ikiwa Messi atalazimika kulipa faini badala ya kifungo alichohukumiwa na mahakama ndipo itajulikana kiwango cha fedha ambacho atalazimika kulipa.

Huku mwendesha mashtaka akipendekeza kubadilisha kifungo hiki kwa faini ya fedha sawa na Yuro € 255,000 Ambayo itakuwa ni sawa na na € 400 kwa siku zikihesebiwa zile angetarajiwa kukaa gerezani.

Messi, pamoja na babake Jorge, walipatikana na hatia ya kuilaghai Uhispania jumla ya €4.1m kati ya 2007 na 2009.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mahakama mjini Barcelona iligundua kwamba walitumia maeneo salama kwa ulipaji kodi Belize na Uruguay ili kukwepa kulipa kodi.

Kando na huku hiyo ya kifungo jela, nyota huyo wa klabu ya Barcelona pia alitozwa faini ya €2m na babake €1.5m.

Walijitolea kulipa €5m “kama malipo ya kufidia”, kiasi ambacho ni sawa na kiasi cha kodi ambayo anadaiwa kukwepa kulipa pamoja na riba, Agosti mwaka 2013.

Rufaa ya Messi dhidi ya hukumu hiyo ilikataliwa na Mahakama ya Juu nchini Uhispania mwezi jana, ingawa muda wa babake kusalia gerezani ulipunguzwa kwa sababu alikuwa amelipa kiasi fulani cha kodi.

Siyo lazima kwa Messi kukaa gerezani kulingana na sheria za Uhispania zinazoeleza kwamba hukumu ya kifungo chini ya miaka miwili kinawezafanywa kama kifungo cha nje yaani bila kuhitajika kukaa gerezani.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.