Swahili
HABARI MPYA

Mahakama imehakikisha mfalme Kigeli V kuzikwa Rwanda

Mahakama ya jimbo la Virginia huko Marekani imesema kua mwili wa marehemu mfalme Kigeri V Ndahindurwa atapelekwa kuzikwa Rwanda katika wilaya ya Myanza (Mwima)

Mwendesha mashtaka ameamua hayo baada ya kuwasikiliza washaidi mbalimbali wa familia ya mfalme na ndio akaamua kua mazishi yatafanyika Rwanda mahali alipo pewa madaraka ya ufalme.

Mabishano yalizuka kwa kua mbele mfalme kufariki hakuandika lolote linalohusu mahali atakapozikwa baada ya kufariki, na siku ya kwanza mahakamani mwendesha mashtaka aliwasikiliza waliopenda apelekwe Rwanda na wengine wapingao kama vile husema sauti ya Markani.

Pamoja na wasaidizi wa pande zote mbili, ilionekana kua hitaji la mfalme lilikua kurejea na kuishi nchi yake Rwanda kwani hakua na utaifa mwengine.

[ad id=”72″]

Christine Mukabayojo, Mfalme Kigeli V ni mjomba wake aliomba mahakama kutimiza hitaji la shangazi yake Speciosa Mukabayojo, la kupelekwa Rwanda kwani ni yeye anayebaki kati ya waliozaliwa pamoja na mfalme ijapo kuwa Emmanuel Bushayija, yeye husema kwamba mfalme alinyimwa fursa ya kurejea nchini mwake kama mfalme eti kwa hayo haone sababu ya kumupeleka Rwanda.

Baada ya kuwasikiliza wote, mwendesha mashtaka alikubali waliokua kwa upande wa dada yake na mfalme kwani ni yeye aliye kua na uhusiano wa karibu na yeye, na ndipo akaamuru kupelekwa Rwanda.

Boniface Benzinge aliye kuwa katibu wa mfalme aliambiya sauti ya Marekani kama hana la kusema waongee na msaidizi wake.

Pasta Ezra Mpyisi, ambaye aliishi pamoja na mfalme yeye eti ana uwajibu wa kuwakusanya wandugu ambao wamejitenga vipande na kua na uhusiano mwema.

Kigeli V Ndahindurwa alitawala Rwanda tangu mwaka wa 1959 hadi 1961, alifariki tarehe 16 Oktoba 2016.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com