Swahili
HABARI

Maelezo Kuhusu maisha ya wagombea urais Rwanda

Karatasi ya Kupigia kura

Leo hii wanyarwanda wanachagua rais atakayewaongoza katika muhula wa miaka saba ijayo. Wagombea hao ni pamoja na Paul Kagame wa chama cha RPF, Dkt. Frank Habineza na Mpayimana Phillipe.

Yaha ni maelezo kuhusu maisha yao

Dkt. Habineza Frank

Ni mwenyekiti wa chama cha Green cha Kupambania Demokrasi na Mazingira(DPGR).Ni mnyarwanda mwenye umri wa miaka 40 aliyezaliwa uhamishoni nchini Uganda sehemu za Mityana na ambapo alisomea shule za msingi hadi mwaka 1991. Alimaliza masomo yake ya shule za Sekondari mwaka wa 1998.

Baada ya hapo aliendelea na masomo ya chuo mwaka wa 1999 hadi mwaka wa 2004 akifuata masomo ya siasa na utawala( Political Admistrative sciences) kwenye chuo kikuu cha Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baada ya kumaliza masomo kwenye chuo kikuu cha Rwanda aliendelea na masomo ya ziada nchini Swideni na Afrika Kusini

Alikuwa mwanaharakati wa mazingira wakati alipokuwa anasoma kwenye chuo kikuu cha Rwanda( UNR) alipoanzisha klabu ya kutunza mazingira “ Rwanda WildLife Clubs”.

Baada ya kumaliza masomo yake aliteuliwa ni kikao cha mawaziri kuwa mshauri maaum wa wizara ya Mashamba, Mazingira, nishati ya Maji na Madini.(Personal Assistant to the Minister of Lands, Environment, Water, Forestry and Mines) mwaka 2006.

Alikuwa hata Kiongozi mkuu wa mradi wa kutunza maji ya mto Nile.

Frank Habineza Alianza shughuli za siasa mwaka wa 2009 alipounda chama cha siasa akishirikiana na watu wengine wachache ambapo walikuwa na lengo la kushiriki uchaguzi mkuu wa 2010 na huku chama chao kikataliwa kusajiliwa.

Baada ya uchaguzi wa 2010 Frank na familia yake walikwenda uhamishoni nchini Swideni na hapo mwaka wa 2011 alitunukiwa taji la mwanaharakati wa demokrasia.

Mwaka wa 2012 ndipo aliporudi kuandikisha chama chake ili kiweze kushiriki uchaguzi wa wabunge wa 2013 na hapo wakashindwa kwa sababu ilikuwa imechelewa kidogo.

Alipewa shahada ya Uzamivu wa heshima na Bethel College ya Indiana nchi ya Marekani kwa kuwa mwanaharakati wa demokrasia.

 Kagame Paul

Kagame Paul alipata fursa ya kugombea muhula wa tatu baada ya kura ya maoni iliyotokea kuibadili katiba.

Amezaliwa mwaka 1957 tarehe 23 Oktoba katika wilaya iliyokuwa ya Tambwe katika Ruhango ya sasa. Amekuwa akiitawala Rwanda tangu mwaka 2000 kama rais wa mpito ambapo alichaguliwa rasmi mwaka 2003. Lakini hapo awali tangu 1994 mara tu baada ya kushinda vita vya ukombozi alikuwa makamu rais wa Pasteur Bizimungu aliyejiuzuru mwaka wa 2000.

Rais Kagame alikulia nchini Uganda wilaya ya Toro ambapo alifika mwaka 1961

Alisomea shule za msingi hapo hapo na shule za sekondali kati ya mwaka wa 1972 hadi 1976 kwenye shule za Ntare School na Kampala Old School. Akiwa na miaka 22 alijiunga na jeshi la waasi waliokuwa wanaongozwa na Yowei Kaguta Museveni ambalo liliangusha utawala wa Idi Amini Dada.

Major Kagame Paul alikuwa mwanajeshi wa kuheshimiwa katika jeshi la Uganda katika idara ya upelelezi na ujasusi.

Alikwenda Umarekani mwaka wa 1990 kufuata masomo ya kijeshi ya  chuo na akarudi baada ya aliyekuwa kiongozi mkuu wa majeshi wa RPF kufariki kwa kuchukuwa uadhifa wake na kuongoza majeshi katika vita vya ukombozi vilivyokamilika mwaka wa 1994 pamoja na kusimamisha mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.

Tarehe 19 Julai mwaka 1994 ndipo Kagame alipokuwa makamu rais hadi kwaka 2000. Toka mwaka huo alikuwa rais wa mpito kabla ya kuchaguliwa rasmi mwaka 2003. Mwaka wa 2010 napo rais Kagame alishinda uchaguzi wa kuongoza kwa muhula wa pili ambako na sasa inaonekana kuwa atashinda uchaguzi na kutawala kwa muhula wa tatu baada ya mabadiliko ya katiba ya 2015 yaliyofuata maombi ya wananchi wakimtaka Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu. Alimwoa Jeannette Kagame mwaka wa 1989 ambaye walizaa watoto wanne.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mpayimana Philippe

Mpayimana Philippe ambaye ndiye mgombea huru pekee ana umri wa miaka 47 ameoa na ana watoto wa tanu. Alizaliwa eneo la kusini wilaya ya Nyaruguru.

Alisomea sekondari kwenye shule la (Groupe Scolaire ya Save). Alisomea chuo kikuu cha Rwanda baadaye na hata Nyakinama na aliendea na masomo yake nchini Kameruni katika masomo ya Lugha na uchambuzi wake.

Baadaye Mpayimana aliendelea na masomo ya utangazaji habari na alifanyakazi kama mtangazaji habari kwenye Televisheni ya Rwanda na yuko miongoni mwa waliotangulia hapo mwanzo wake mwaka wa 1992.

Alikuwa mhamiaji kwenye nchi nyingi na ndipo alipopata wazo la kuandika kitabu chake cha “Réfugiés rwandais, entre marteau et enclume : récit du calvaire au Zaïre”.

Mpayimana alirudi Rwanda mapema mwezi Januari 2017  akiwa ana lengo la kukusanya nyaraka zote alizokuwa anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwania kiti cha urais wa Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com