kwamamaza 7

Madereva kutoka Tanzania walalamikia huduma mbaya wanayopata nchini Rwanda

0

Madereva wa magari makubwa yenye mizigo kutoka nchini Tanzania wametangaza kuwa na malalamishi ya huduma mbaya wanazopatiwa kwenye mpaka kati ya Rwanda na DR Congo, wilayani Rubavu, magharibi kaskazini mwa Rwanda kutokana na kutokuwa na mahali pa kulala, maji, chakula ,wala hospitali.

Mmoja wao kwenye mazungumzo na Sauti ya Marekani , ameeleza wanapata taabu sana wanapofika mjini Rubavu na kuwa maisha yao huwa hatarini kutokana na uhaba wa mahitaji ya msingi.

“ Hali  hii hapa hakuna sehemu ya kujificha  kwa mvua wala jua. Ni hatari kwa kiujumla.Hapa hakuna huduma ya chakula, hakuna mahali pa kutibu watu,tunaomba serikali kutayarisha haya mambo kama ilivyofanyika pengine kama vile Rusumo na mjini Kamembe. Tunahitaji mambo ya msingi kama maji, mahali pa kulala,chakula. Isipokuwa mwenyezi Mungu, sisi hatunasehemu ya kukimbilia”

Mwenzake ameongeza hali yao ina kuwa ngumu hususani wakati wa mvua.

“ Kama mtu ana mkeka tunatandika na  tukalala, mvua inaponyesha hatuwezi kulala tunaamka kuchunguza vyakula kama vile unga kisiharibike. Kuna wale ambao wanakaa hapa wiki au  mwezi mzima”

Makamu Kiongozi wa Wilaya ya Rubavu kwa wajibu Maendeleo ya Kiuchumi, Janvier Murenzi ameeleza serikali haikujenga hiki kituo kutokana na kuwa kuna mradi mwingine utakapoanzishwa hapo.

“ Kile ni kituo cha mpito, mji wetu una hoteli, lodge na kutaanzishwa maji huko lakini ni mpito”

Madereva wameitaka serikali ya Rwanda kujenga nyumba za kushushia mizigo ili kupunguza siku wanazokaa huku wilayani Rubavu kwani mahali pa kulala ni bei ghali mno.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.