kwamamaza 7

Mabunge wamekubali Kiswahili kama Lugha rasmi Rwanda

0

Tarehe 8 Februari 2017, mabunge walikubali mradhi wa sheria unaokubalia Lugha ya Kiswahili kama lugha inayokubaliwa na sheria Rwanda na kuwa ilikubaliwa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rwanda kama nchi ya jumuiya ya Afrika ya Mashariki EAC, imeitia lugha hio katika lugha rasmi yenye kukubaliwa na sheria ya Rwanda iliyotiwa mhuri 2003 na ikasahihishwa 2015 hadi sasa, na hayo ni baada ya kuchunguza ya kuwa nchi ambazo huunda Afrika ya Mashariki hutumia Lugha hio.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri wa michezo na utamaduni, Uwacu Julienne alifasiria umuhimu na usamini wa lugha ya Kiswahili na hakutakuwa matokeo mabaya kwa ajili ya kutumia Kinyarwanda kwa kuwa yote itatumiwa nchini, eti “ Kinyarwanda kama lugha ya ukoo wa nchi itaendelea kuzingatiwa”.

Hata kama Mradhi umekubaliwa, Januari 2017 wakuu wa nchi za Afrika ya mashariki EAC walikubalia kutumia passeport moja, na kuandikwa katika lugha ambazo itaongezeka Kiswahili na kutumikishwa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Lugha ya Kiswahili ilikuwa ikizungumzwa katika nchi 12 za Afrika, na kwa kuwa imekubaliwa katika nchi za Afrika ya Mashariki, haraka sana itafundushwa hata shuleni.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.