kwamamaza 7

Mabalozi wapinga hatua ya Tume ya Uchaguzi ya Rwanda dhidi ya Wagombea Urais

0

Mabalozi kutoka nchi za Ugaibu wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hatua ya Tume la uchaguzi nchini Rwanda (NEC) ya kuwa wagombea urais wataruhusiwa kupitisha maoni yao kupitia tovuti za kijamii baada ya kuchunguzwa.

Mabalozi hawa wanasema hivi baada habari hii imekwisha enea katika vyombo kadhaa vya habari vya nchi na kimataifa.

“Sisi wote tuna wasiwasi kuhusu hatua hii na nadhani ni muhimu kujua lengo la hatua hii, mimi ni naweza kusema kwamba inalenga kuvunja uhuru na haki ya maoni” Balozi wa Marekani nchini Rwanda Erka, Bargles -Ruggles asema.

Balozi huyu ametangaza mambo haya wakati wa mazungumzo kuhusu Haki za Kibinadamu yaliyoandaliwa na Umoja wa Ulaya, na kuhudhuriwa na Mabalozi mbalimbali na hata waziri Haki Johnston Busingye.

Hatua hii ya kuchunguza ujumbe unaopitishwa na wagombea urais kupitia tovuti za kijamii itaanza kutekelezwa kutoka 14 Juni wakati ambapo mbio za uchaguzi zinasubiriwa kuanza.

Hatua hii inafafanua kwamba ujumbe, picha ama vyombo vingine vya ajili ya kampeni ya uchaguzi vitapishwa kwanza katika Tume la Uchaguzi masaa 48 kabla ya wakati vinavyotarajiwa kutumiwa.

Kiongozi wa Tume hiyo alieleza kwamba hatua hiyo inalenga kupambana na maneno na vitendo ambavyo vinavyoweza vunja usalama wakati matatizo yaliyoachwa na ubaguzi ambao Rwanda ilipitia yangali hai.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Balozi wa Ujerumani nchini Rwanda, Peter Woeste, alisema kwamba nchi nyingine zilikabiliwa na tatizo kama hili lakini akajiuliza ikiwa kuchunguza ujumbe ingekuwa hatua sawa, Kwa mjibu wa taarifa ya News 24.

Mwanasiasa mmoja wa upande wa upinzani alipinga hatua hii akidai kwamba inalenga kumzuia yeyote atakaempinga Rais Kagame ambaye anatarajiwa kuania muhula wa Tatu.

Mpaka sasa kuna wagombea huru wane waliokwisha tangaza nia yao ya kugombea kiti cha urais wakiwemo: Mwenedata Gilbert alieshindwa wakati alipoania kiti cha ubunge mwaka 2013.

Halafu, kuna Diane Rwigara, binti wa marehemu mwanamali Assinapol Rwigara, aliefariki kifo cha ajali mwaka 2015.

Mwingine ni Philippe Mpayimana, mtangazaji wa zamani alierudi Rwanda kutoka uhamisho kule Ulaya.

Mwishoni, ni Dr Frank Habineza kiongozi wa Chama cha upinzani, Green Party.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.