kwamamaza 7

Mabaki ya Maiti 849 za waliouawa katika mauaji ya kimbari dhidi ya watusi yazikwa

0

Mabaki ya maiti 894 ya waliouawa katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi kutoka mahali tofauti pa kumbumbu yazikwa kwenye Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Nyarushishi iliyoko tarafa ya Nkungu wilaya ya Rusizi.

 

Utaratibu huu ambao ulijumuisha waheshimwa mbalimbali akiwemo Dr Bizimana Jean Damascene, katibu mtendaji wa Tume ya Kupambana na itikadi ya mauaji ya Kimbari( CNLG).Utaratibu huu ulifanyika tarehe ya 23 Juni 2017.

Kiongozi huu alisema kwamba kuhamisha mabaki ya maiti katika Kumbukumbu nyingine ni kulingana na mfumo wa kuhifadhi ishara za mauaji kwa muda mrefu, na hii itarahisisha kutunza Mahali hapo pa kumbukumbu.

Munyura Jean Pierre, mmoja wa waliokuwa na maiti ya mtu mwenzake aliyezikwa hapo, alisema kwamba manusura wenzake hawakuwa wanaelewa umuhimu wa utaratibu huu lakini kwa sasa wameanza kuuelewa. Harelimana Frédéric, Meya wa Wilaya ya Rusizi ,alisema kuwa kuna maiti 86 ambazo hazikuzikwa kwa kuwa wamezikuta zikiwa hazijaharibika sana, zimekuwa zikionekana kama zilizozikwa wiki mbili awali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katika siku hii, ushiriki wa Ufaransa katika mauaji haya umegusiwa, hapa kukifafanuliwa kwamba walipanga kambi ya watutsi sehemu za Nyarushishi wakiwadanganya kwamba ni kwa ajili ya kuwalindia usalama na hapo kundi la wanamgambo (interahamwe) wakaja wakachukuwa baadhi yao na kuwaua wakafanya hivyo siku kwa siku huku wafaransa wakikaa bila kufanya kitu.

Mukama  Abbas, Makamu Mwenyekiti wa bunge baraza la wabunge amempongeza Kagame na majeshi waliokuwa wa RPF Inktanyi kwa kuwa walijitolea na kusitisha mauaji haya na kutokana na hivyo Rwanda inaishi kwa usalama salamini.

“ Historia haizeeki kutakuwa wakati ambapo, Wafaransa watatakiwa kujibu haya. Utawala unabadilika siku kwa siku, wakati kutakuwa na utawala ambao utaelewa ushiriki wa wafaransa katika maafa haya, tuna imani kutakuwa kutendewa kwa haki mahakamani” asema

Maiti hizi zilizozikwa siku hii ni nyongeza kwa zingine 1500 zilizozikwa mwaka uliopita.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.