Home HABARI MPYA Maandalizi ya kuunda serikali ya Rwanda wakiwa ukimbizini huendelea
HABARI MPYA - February 15, 2017

Maandalizi ya kuunda serikali ya Rwanda wakiwa ukimbizini huendelea

Baada ya kushindwa kuwasili Rwanda mara ya pili, ili kuandaa kuwania uchaguzi wa uraisi, kiongozi wa chama cha upinzani “ISHEMA”, Padri Nahimana anasema ya kuwa ataunda serikali ambayo itatumikia ukimbizini na maandalizi huendelea.

Taarifa husema ya kwamba tarehe 23 Januari 2017 wangelikuja Rwanda kuandikisha chama chao ISHEMA ili wapate ruhusa ya kuwania uchaguzi wa urais utao fanyIka mwaka huu wa 2017. Wanasema pia kuwania urais si kutafuta uongozi ao utawala ila lengo lao ni “kuunganisha Wanyarwanda ili waweze kujenga Rwanda yenye maendeleo”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baada ya kushindwa kufika Rwanda, chama hiki husema ya kwamba wamekamata mipango miwili mikubwa, ya kwanza ikiwa mahakamani, ya pili ikiwa kuongea na raia wanaohitaji mabadiliko ili kuunga serikali itayo tumikia ukimbizini yenye kuwa na majukumu ya kuondoa utawala wa Rwanda.

Baada ya siku 15 ya maongezi pamoja na wanaohitaji mabadiliko, chama ISHEMA husema ya kuwa maongezi yalipitika vema na kukapitakana walio kubali kuunda serikali ukimbizini, wengine walikubali wazo ila hawakukubali serikali ya ukimbizini na wengine walionyesha ya kuwa hawakukubali wazo hilo hata kidogo.

Tangazo lililo tiwa mhuri na Padri Nahimana, anasema ya kuwa jioni ya tarehe 17 hadi 19 Februari 2017, mjini Paris, nchi Ufaransa kutakuwa mkutano wa wale walio kubali kuunda serikali itayo tumikia ukimbizini, na majina ya watakayo kuwa katika serikali na kanuni zao vitatangazwa tarehe 20 Februari 2017.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.