kwamamaza 7

Maafisa wa polisi 26 wafukuzwa daima kupitia mwaka wa 2016

0

Polisi ya Rwanda imewapiga marufuku milele maafisa wa polisi 22 kwa ajili ya kushiriki na rushwa na wengine 4 ambao walifukuzwa kwa sababu ya tabia ambazo hazilingani na maadili pamoja na kanuni za polisi ya Rwanda.

Ripoti nyingi zilitolewa na sehemu ya Rwanda ya taasisi ya kimataifa ya kuhifadhi uwazi na kupambana dhidi ya rushwa, Transparency Interntional Rwanda; husema kwamba katika polisi kunapatikana rushwa kwa kiwango cha juu ijapokuwa polisi hukana madai hayo kwani watuhumiwa hufanya pekee, hawakutumwa na polisi.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Miongoni mwa hawa 22, kuna walioperekwa mahakamani ili kuhukumiwa kuhusu dhambi ya rushwa na wengine wasiogunduliwa kama wanakuwa na hatia; lakini wote hawakuruhisiwi kurudi kazini.

Kiongozi wa polisi wa kuhusika na usalama wa barabarani, CP George Rumanzi alieleza kuhusu maafisa ambao mahakama amethibitisha kuwa hawana hatia lakini hawakurudishwa kazini.

Alisema kwamba ijapokuwa mahakama yamethibitisha, hawakukubaliwa kurudi katika polisi ya Rwanda kwa sababu ya kutopea heshima kanuni mbali mbali.

Miongoni mwa tabia zilisababisha kufukuzwa kwa maafisa wengine (4) kuna ulevi, ukahaba n.k.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Maafisa wengine 54 walipewa adhabu za kikazi lakini hawakupigwa marufuku bali bodi ya nidhamu katika polisi ya Rwanda imepata maamuzi kulingana na ukali wa makosa walifanya.

Utafiti wa Transparency International Rwanda katika 2015, ulionyesha kwamba shirika za polisi ya Rwanda zilichukuwa nafasi ya kwanza kwa kuhusika na rushwa kwenye kiwango cha 6.3%.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.