kwamamaza 7

Maadhimisho ya mauaji ya kimbali  ni ukweli unaokuenda pamoja na kuijenga nchi-Rais Kagame

0

Rais Paul Kagame wakati wa kuanzisha wiki ya maadhimisho ya mauaji ya kimbali  dhidi ya Tutsi mwaka 1994 amesema kuwa  jambo hili ni ukweli unastahili kuenda pamoja na kuijenga nchi.

Katika hotuba yake,Rais Kagame ameeleza kuwa ukweli huu unaenda pamoja na kujenga uwezo wa Wanyarwanda na kuwa wale ambao hawakumbuki wanapuuza yaliyotokea katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

“Ukweli ndio msingi wa maendeleo,tunapokumbuka tunakumbuka huo ukweli na wale ambao hawakumbuki wanapuuza huo ukweli…maadhimisho yataendelea,tutajenga nchi yetu kuanzia sisi wenyewe”

Rais amewakumbusha Wanyarwanda kwa ujumla kuwa maadhimisho ya mauaji ya kimbali ni jambo la kupambana na historia ya raia hasa kuna mambo ya kutekelezwa ili mabaya haya yasitokee tena.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Maadhimisho ni tabia yetu,familia zetu,nchi yetu.Maadhimisho ni kupambana na historia yetu.Hili linatukumbusha kuwa tusipochunga vizuri haya yanaweza kutokea tena.Yanatukumbusha wajibu wetu wa kupambana vilivyo na historia hii”.

Maadhimisho ya mauaji ya kimbali dhidi yaTutsi mwaka 1994 yanatokea mala ya 24 ambako kunakumbukwa zaidi ya Watutsi miliyoni moja waliouawa.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.