kwamamaza 7

Lugha za Kiswahili na Kinyarwanda miongoni mwa lugha 10 zinazotumiwa na watu wengi barani Afrika

0

Miongoni mwa lugha 2000 zinazotumiwa barani Afrika Kiswahili na Kinyarwanda kama lugha za Afrika ya mashariki ni lugha ambazo zinazopatikana katika lugha kumi mtawalia zenye kutumiwa na watu wengi ambapo Kiswahili kinatumiwa na watu kati ya milioni 150 na 100 huku Kinyarwanda kikatumiwa na takriban watu milioni 20.

Kiarabu ndio lugha inayoongoza ikiwa na watu milioni150, Kiswahili milioni(100), Amharic milioni(50), Kihausa milioni(35), Kiyoruba(30), Ki-Oromo milioni(25), Ibo milioni(24), Kinyarwanda na Kirundi milioni(20), Lingala milioni( 13) Kizulu na Kixhosa (10-8).

Kiswahili kama lugha yenye kutumiwa na watu wengi, hutumiwa na karibu watu wote wa Afrika ya mashariki, na nchi nyingine 10 za Afrika ambazo baadhi yazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (jimbo tano za Kongo ya mashariki) Mozambique, u Rwanda, Uganda, u Burundi, Tanzania, Kenya na Somalia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kiswahili ni lugha ambayo kihistoria ilieenea kwa sababu ya waarabu ambao walikuwa wakifanya biashara yao katika nchi za afrika ya mashariki husuasani pwani Tanzania (Zanzibar) na hiyo kuipa hadhi ya kuwa na maneno mengi ya Kiarabu, Kiswahili sanifu yenyewe ni lahaja ya Zanzibar huku zikihesabiwa lahaja nyingine za Kiswahili ikiwemo nyingine ya Kongo inayojulikana kama kingwana hii nayo iliyoletwa na wafanyabiashara waliokuwa wakajiita Wangwana na kufanya lugha yao kubeba jina la kingwana.

Kiswahili mpaka sasa ni lugha inayozidi kunea kwa sababu na hata vyuo mashuhuri mfano wa Havard ya Marekani na Oxford ya Uingereza vilianza masomo ya lugha hii. Muungano wa Afrika (AU) ilitangaza hata Kiswahili kama lugha rasmi .

Lugha ya Lingala nayo ilipata umarufu wake kutokana na mdundo wa mziki wa Lumba na hii kuifanya kuenea katika pande zote za dunia na pia kulingana na wingi wa raia wa kongo wanaoishi karibu duniani kote. Lingala inatamkwa na takriban milioni 13 za watu kwa mjibu wa RFI.

Lugha ya Kinyarwanda na hata Kirundi ambazo huchukuliwa kama Lugha moja kwa sababu ya urahisi wa mawasiliano kati ya watu wanaoongea lugha hizo mbili. Lugha hizo hutamkwa na watu takriban milioni 20 kutoka nchi za Burundi,Rwanda, Uganda hususani kusini, mashariki ya DRC na hata sehemu ndogo ya Tanzania.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.