kwamamaza 7

Lugha ya Kiswahili kukubaliwa rasmi nchini Rwanda

1

Mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika tarehe 12 Oktoba 2016 umetoa suluhisho mbali mbali za kuridhisha katika shughuli za selikali ya Rwanda. Katika makala ya 6 ya maamzi ya Mkutano huo, walitoa uamzi wa lugha ya Kiswahili kukubaliwa kama lugha rasmi nchini Rwanda.

Taarifa hio ilikuwa ikisema kwamba mkutano wa baraza la mawaziri imetoa mradi wa sheria wa ‘utumiaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi baada ya kuchunguza vizuri’.

Mradi huu utapitishwa na wabunge ili kutekelezwa.

Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi inayozungumzwa duniani kwa kiasi kikubwa hasahasa katika eneo la  Afrika ya Mashariki na hutumiwa kama lugha rasmi katika Jumuiya ya Afrika ya mashariki (EAC).

Serikali ya Rwanda imetia bidii ili kuimarisha lugha ya Kiswahili ndio maana ya mpango wa kufundisha Kiswahili katika shule za sekondari. Wizara ya Elimu ya Taifa ilianzisha kitengo cha kiswahili katika Taasisi ya Elimu ili kiweze kushughulikia vema ufundishaji na ukuaji wa Kiswahili kwa kuwekwa mkondo wa lugha hii, EKK (English-Kiswahili-Kinyarwanda).

Kiswahili kimeunga mkono lugha nyingine rasmi katika serikali ya Rwanda yaani Kinyarwanda kama lugha ya taifa na Kiingeleza pamoja na Kifaransa zinazotumiwa katika shuguhuli za serikali.

Katika nchi za majirani, Kiswahili kinatumiwa kama lugha ya taifa, lugha ya shule za msingi, lugha ya serikali na mahakamani nk…, Ijapo katika Kenya ni lugha ya taifa lakini kiingeleza ni lugha rasmi ya kiutawala. Kiswahili kimetangazwa kuwa lugha ya kitaifa tangu 2005 nchini Uganda.

Théogène U @Bwiza.com

1 Comment
  1. Théogène BAYAVUGE says

    Ni kitu kizuri kusikia kuwa kiswahili kimekubaliwa kama lugha rasmi nchini Rwanda. Ninafikiri sisi wazungumzaji wa Kiswahili tutafaidika kabisa.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.