kwamamaza 7

Ligi ya “Azam Premier League Rwanda” yamalizika Kiyovu Sports wakishushwa daraja huku

0

Ligi ya soka ya Rwanda imemalizika jana tarehe 15 mwezi Juni ikiziacha timu kali Kiyovu Sports na APR FC na msimu mbaya huku mahasimu wao Rayon Sports wakisherehekea Ubingwa walioshinda hivi karibuni mwezi jana.

Baada ya miaka 50 wakichezea daraja la kwanza , Kiyovu Sports washushwa daraja na mahasimu wao wa zamani Rayon Sports baada ya kuchapwa mabao 2-1. Mechi hii ilipigwa Uwanja wa Mumena mbele ya mashabiki wengi wa Rayon Sports kama kawaida. Mashabiki wa Kiyovu pamoja na wachezaji wa zamani wa timu hii nao walikuwa wakishuhudia kwa majonzi timu yao ikichapwa na masimu Rayon Sports ambao hawakuwaonea huruma.

Timu nyingine ambayo ilipata pigo msimu huu ni APR FC ambayo haikuweza kushika hata nafasi ya pili kwa ajili ya tiketi ya kuakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

APR FC ililazwa na Bugesera FC mabao 2-1.

Matokeo yote:

  1. APR FC 1-2 Bugesera
  1. Police FC 4-2 Marines
  2. Musanze 1-0 Sunrise
  1. Mukura VS 0-1 Kirehe FC
  1. Gicumbi FC 1-3 Pepiniere
  2. Espoir 0-1 AS Kigali
  3. Kiyovu Sport 1-2 Rayon Sports
  4. Amagaju 0-1 Etincelles

Jedwali ya ligi ya Rwanda “Azam Premia League” ilivyomalizika kwa mjibu wa Ruhagoyacu.com

  N   TIMU MICHEZO MABAO ALAMA
01 RAYON SPORTS 30 43 73
02 POLICE FC 30 24 61
03 APR FC 30 19 57
04 AS KIGALI 30 13 53
05 BUGESERA FC 30 13 50
06 MUSANZE FC 30 2 45
07 ETINCELLES FC 30 -4 40
08 ESPOIR FC 30 2 39
09 SUNRISE FC 30 -5 33
10 AMAGAJU FC 30 -8 33
11 KIREHE FC 30 -6 32
12 MUKURA VS 30 -14 32
13 MARINES FC 30 -15 30
14 GICUMBI FC 30 -21 28
15 KIYOVU SPORTS 30 -16 27
16 PEPINIERE FC 30 -27 17

 

Baada ya ligi kumalizika kunasubiriwa timu gani ambayo atakuwa mshindi wa Peace Cup ambayo APR inapaswa kufanya kila lolote lasivyo mashabiki wa Rayons Sports wataendelea kuwazomea.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.