Swahili
HABARI MPYA SIASA

Kwa siku yake ya 10 ya Kampeni Rais Kagame aendesha Kampeni wilaya za Kirehe Ngoma na Rwamagana.

Paul Kagame ambaye ni mgombea wa chama cha RPF anaendelea na ziara zake za kampeni ambako kwenye siku yake ya 10 amezifikia wilaya za Kirehe, Ngoma hatimaye Rwamagana.

Kampeni  ya Kirehe

Paul Kagame, kama ilivyokuwa kwenye wilaya nyingi alizokwisha zipitia alipokewa na watu wengi sana waliokuja kushiriki mipango yake na kumwonyesha kwamba watamwunga mkono kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao.

Wananchi wa Kirehe

Paul Kagame alipokuwa akihotubia kwa waliohudhuria shughuli za kampeni yake ameahidi kujenga barabara ya rami mnamo miaka miwili ya kwanza. Aliendelea kusema kwamba yote yalifikiwa kwa umoja na ushirikiano wa wanyarwanda na kuwa iliwezesha kumpa heshima mwanamke mnyarwanda.

Kampeni za Ngoma

Alipofika wilaya hii alisema kwamba anafuraha nyingi kuwaona wakijumuika kwa wingi na kusema kuwa wanapojumuika Inkotanyi mungu huwatembelea.

Hapa aligusia kuhusu mipango yake kwa kusema kuwa wanachi wa Ngoma wataendelea kupata maendeleo mengi ikiwemo barabara itakayowaunganisha na wilaya ya Nyanza na Bugesera. Aliendelea kusema kuhusu mji wa ngoma ambao amesema hauna muonekano wa kumfurahisha.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“mlikwisha yafikia mengi mlifuga, mkalima, mkajenga miundombinu na mengineyo, lakini ningependa msaada wenu kuyafikia ya ziada. Mnaona mji huu wa Ngoma ningependa kuubadili muonekano wake. Baada ya tarehe 4 Agosti, mwanzo utakua hapo hapo na kuanza kuongea na ngazi husika jinsi ya kubadili muonekano wa mji huu” asema.

Aliendelea kuwahimiza kumchagua yeye kama mgombea wa chama cha RPF ili yote yaje yakatimizwa na kusisitiza kwamba angehitaji maendeleo ya nchi nzima yasiyomwacha nyuma watoto,vijana, wanawake, wanaume na waze wote wakichangia.

Aligusia pia umoja unaowafanya kufikia hayo yote na kusema kwamba kujiunga kwa RPF na vyama vingine ndio ishara halisi ya umoja unaowafanya kuyafikia malengo.

Baada ya Hapo aliendelea wilaya ya Rwamagana

Kampeni Rwamagana

Alipowasili Rwamagana alikaribishwa na raia wengi kama inavyokuwa kwenye wilaya anazokwenda kuendesha kampeni. Ameanza hotuba yake ya siku kwa kuwashukuru kwa kushiriki shughuli hizi zilizofanyika wilaya ya Rwamagana na kuongeza kwamba yeye anaishi mpaka wa wilaya ya Kayonza na Rwamagana. Alisema kwamba historia ya nchi na vitendo vyake ndivyo vitakaowawezesha kujiendeleza na kuijenga nchi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ameongeza kwamba tarehe 4 Agosti ndiyo itakaowapa chanzo cha kuendelea na mipango yao ya kujiendeleza kwa kuondosha matatizo yanayowakumba wanyarwanda kama maradhi ya lishe kwa watoto.

Aligusia kwamba umoja na ushirikiano wa wanyarwanda ndio utakaowawezesha kuyafikia haya yote kwa haraka iwezekanavyo kwa mfano wa vyama vilivyojiunga na RPF Vikiwa na lengo la kuiendeleza nchi.

Amekamilisha kwa kuwatakia heri na fanaka na kuwakumbusha kwamba tarehe 4 Agosti ndio tarehe ya maamzi na kwamba wanahimizwa kumaliza kazi mapema.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com