kwamamaza 7

Kwa mala ya kwanza ugonjwa wa Ebola wakaribia Rwanda

0

Ugonjwa wa Ebola umekaribia nchi ya Rwanda kwa  kilomita 370, mkoa wa Beni nchini DR Congo.

Taarifa hizi zimekaribishwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Gisenyi, Luteni Kanuni Dk. Kanyankore William kwa kusema kwa sasa  Ebola imejitokeza karibu na Rwanda kutoka kilometa 1070.

Huyu ametangazia vyombo vya habari kuwa  hili limezusha wasiwasi mno kutokana na kuwa kuna wafanyabiashara kutoka huko  Butembo na Beni wanaoenda nchini Uganda na kuja  nchini Rwanda kupitia mpaka wa Cyanika.

Kwa hiyo, Daktari Kanyankore amewahamasisha wakazi kutoa habari husika na huu ugonjwa.

Serikali ya DR Congo  mwezi uliopita ilitangaza kuna wagonjwa wa Ebola maeneo ya Mkoa wa Kivu Kaskazini kama vile Mangina na Mabalako na Ituri karibu na Uganda.

Tangu  tarehe 15 Ogasti  kuna takwimu za wagonjwa wa Ebola 51 pamoja na 44 waliofariki.

Utafiti wa Shilika la Ki mataifa la Afya ( OMS) ulionyesha kwamba Ebola ilionekana mala 10 nchini DR Congo.

Hili linasababishwa mala nyingi na raia ambao wanakula wanyama  kama vile sokwe nchini DR Congo.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.