kwamamaza 7

Kusini:Teknolojia kupunguza gharama ya elimu

0

Matumizi ya teknolojia ya utandawazi ICT katika wilaya za Huye na Nyanza,kusini mwa nchi yatowa fursa kwa elimu ya vyuo vikuu na kupunguza gharama ya elimu.

ICT katika wilaya za Huye na Nyanza inazidi kuchangia fursa katika kuinua kiwango cha Elimu ya chuo kikuu kwa wakazi wa maeneo hayo kupitia mfumo wa elimu kwa njia ya mtandao (e-learning).

Tukizungumza na baadhi ya wanafunzi katika vyuo vikuu wilayani Huye na Nyanza wamelezea hisia zao kuhusu mfumo huu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Gislene Umukunzi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili kitengo cha uchumi katika chuo kikuu huria cha PIAS wilayani Huye,amelezea umuhimu wa mfumo huu kwa wanaohitaji kujiendeleza na vyuo vikuu.

 “Ni hatua nzuri kuhamasisha  mfumo huu katika vyuo vikuu hapa wilayani Huye, ili watu waweze kuufahamu vema na kuutumia.Vinginevyo ni mfumo rahisi sana na utasaidia wengi kupunguza gharama za masomo ya elimu ya juu” alisema.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katibu mkuu mtendaji wilaya ya Huye,Vedaste Nshimiyimana amesema  kuwa miongoni mwa watu walioweza kufaidika na mpango wa elimu ya juu kupitia mfumo huo ni pamoja na wafanyakazi kutoka idara za serikali ambao wengi wao wameweza kuhitimu stashahada za juu kupitia mfumo huo.

 Diwani wa Nyanza,Bw Erasme Ntazinda amelezea kuwepo kwa mfumo huu wilayani Nyanza.RMI ni moja ya taasisi za elimu ya juu wilayani Nyanza na kwa mjibu wa Erasme tayari kumeanzishwa mfumo huo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hadi sasa ni vyuo vikuu huria pekee ndio vinatumia mfumo huu katika wilaya za Huye na Nyanza,huku chuo kikuu cha taifa UR-Huye  mpango huu bado haujawa na nafasi.

Mfumo wa elimu ya juu kwa njia ya mtandao tayari umekwisha wafaidisha wafanyakazi kutoka halmashauri za wilaya Huye na idara nyingine za serikali kwa takribani miaka kadhaa tangu mwaka 2005 tokea kuanzishwa kwake wilayani Huye.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Shaban Thabiti/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.