Swahili
Home » Kungekuwa na uizi wa kura sitakubali matokeo- Mpayimana Phillipe
SIASA

Kungekuwa na uizi wa kura sitakubali matokeo- Mpayimana Phillipe

Mpayimana Phillipe ambaye ni mgombea anayewania kiti cha urais katika uchaguzi wa hivi karibuni mwezi tarehe 4 aomba kura kuendeshwa kwa uwazi na amesema kwamba ikitokea kuna uizi wa kura wa namna yoyote hatakubai matokeo.

Amesema haya katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya kampeni zake jana tarehe 31 Julai katika wilaya ya Musanze Jimbo la Kaskazini tarafa ya Muhoza.

Mgombea huyu alisema kwamba ana imani ya kushinda katika uchaguzi na kwamba bila shaka utafanyika katika hali ya uwazi kama ilivyo kwa kampeni. Ameongeza kwamba kinyume na hayo hatakubali matokeo ya uchaguzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“ikiwa kampeni za uchaguzi zinazoendelea kufanyika kwa utulivu na uwazi basi tungependa na uchaguzi kufanyika hivyo hivyo. Sitaweza kuwa na wawakilishi katika kila chumba cha uchaguzi lakini iwe wajibu wa kila mnyarwanda kujua kwamba kuiba ama kupiga kura kwa kushurutishwa haiko halali. Naomba hili lifanyike kama hivi sitaki kusikia kuna popote lilipotokea…”.

Tunataka nchi yenye haki na kwa hivi nitakaposikia kuna popote ilipotokea kuiba kura ama kushuritisha watu kuchagua kusiko kwa maoni yao sitakubali matokeo”.

Mgombea huyu aliwaahidi wananchi wa Musanze kwamba atapambana na kupunguza pengo la uwezo liloko kati ya watu tajiri na maskini nchini Rwanda na kwamba anataka watu wote kunufaika na uchumi wa nchi ili kusiwe na wale watakaodai kuwa maskini tena.

Mpayimana pia aligusia ya kwamba iwapo atashinda uchaguzi ataendeleza kazi ndogo ndogo kwa kuwa yeye aligundua kwamba licha ya kuwa serikali inazipuuza zina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya wananchi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com