Swahili
Home » Kundi la wanamgambo wahaidi watashambulia Rwanda
HABARI MPYA

Kundi la wanamgambo wahaidi watashambulia Rwanda

Kundi la wanamgambo kwa jina la National Liberation Forces (NLF) wamejigamba ndio waliofanya mashambulizi yote ya awali ambayo yaliua watu wawili na kuiba mali ya wakazi na kuwa wanalenga kuipindua serikali ya Rwanda.

Tangazo kwa vyombo vya habari la chama cha Rwandan Movement for Democratic Change (RMDC) ambalo limetupiwa jicho na Chimpreports, linasoma chama kimeunda hili kundi la kijeshi kwa misheni ya kupindua utawala wa Rais Kagame.

Wanamgambo wa NLF wakiwa msituni

“  Kwa hiyo, tumeunda jeshi la NLF na kulipa wajibu wa kupindua serikali ya chama tawala RPF” tangazo linasoma.

“Tutatumia mbinu za vita kuipindia serikali kwani ilikataa njia za amani ” limeongeza

Kuna taarifa kwamba Chama cha RMDC kinaongozwa na Paul Rusesabagina na makamu wake Meja. Sankara Nsabimana Callixte ambaye pia ni Msemaji wa NLF na mwingine Kanuni Wilson Irategeka ambaye ni kiongozi wa kundi kutoka FDLR.

Wanamgambo wa NLF wakisafisha bunduki zao

NLF imetangaza ilishambulia pengi nchini Rwanda pakiwemo kusini mwa Rwanda,wilayani Nyaruguru, Cyangugu, Nyamagabe, Bugesera na Huye ambako ni kusini mwa Rwanda.

Mmoja mwa wanamgambowa NLF akiwa na ‘ machine gun”

Kwa sasa,upande wa serikali ya Rwanda haujafunguka lolote kuhusu haya madai ya wanamgambo wa NLF.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com