Rais wa Rwanda,Paul Kagame

Rais waJamhuri ya Rwanda,Paul Kagame ametangaza kuwa hawana budi Wanyarwanda kufurahia hatua kubwa ya maendeleo iliyopigwa husika na ushirikiano,maendeleo na mangine kwa kuwa haikuwa rahisi kutimiza haya yote.

Kwenye hotuba yake kwenye mkutano kwa jina la’ Umushyikiarano’ Rais Kagame leo tarehe 18 Disemba 2017 amewataka Wanyarwanda kukumbuka makiwa na yaliyomo mwa historia zao na kufanya iwezekanavyo ili kupata maendeleo.

Rais Kagame amesema “Tulipambana na changamoto kadhalika lakini tuliweza kupiga hatua ya maendeleo,tuna nguvu zaidi ya zile tulizokuwa nazo zamani,hatuwezi kubabaishwa na lolote”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande mwingie Rais Kagame amewakosoa wanaolegeza na kuwambia kuna mengi yanayohitaji kutimizwa siku za usoni.

Rais Kagame ameonyesha namna ambavyo Rwanda ilipiga hatua ya maendeleo tangu miaka iliyopita kwenye sekta mbali mbali kama vile mawasiliano,uchumi,ushirikiano,kilimo na nyingine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina