kwamamaza 7

Kujiua kwa mshukiwa wa ugaidi kwazua shutuma Ujerumani

0

Madai ya maafisa wa masuala ya sheria wa jimbo la Saxony nchini Ujerumani kuwa walifanya kila waliloweza kuepusha mshukiwa wa ugaidi Jaber al Bakr kujiua, yamekosolewa na kupokelewa kwa mashaka.

Al Bakr alijiua jana katika chumba alichokuwa akizuiwa katika jela ya Leipzig kwa kutumia shati lake.Waziri wa sheria wa Saxony Sebastian Gemkow amewaambia wanahabari kuwa tukio hilo halikupaswa kutokea lakini lilifanyika na kuongeza daktari wa kushughulikia matatizo ya kiakili aliyemchunguza mshukiwa huyo alibaini hakuna hatari ya al Bakr kujidhuru.

Wanasiasa wa Ujerumani wameghadhabishwa na jinsi kisa hicho kilivyoshughulikiwa na maafisa wa usalama na wa sheria. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas Di Maiziere amesema kujiua kwa al Bakr kumehujumu uchunguzi wa kubaini iwapo alikuwa na washirika au mitandao ya kigaidi Ujerumani.

Raia huyo wa Syria anashukiwa kupanga njama ya kufanya shambulizi la bomu katika uwanja wa ndege wa Berlin.

Kamugisha L@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.