kwamamaza 7

Kuangalia mapenzi ya video kwavuma kusini mwa Rwanda

0

Wakazi  Wilayani  Nyaruguru kusini mwa Rwanda wametangaza kwamba filamu za uchi zinavuma huko na kusababisha kutoelewana katika ndoa.

Suala hili limeathiri sana wanawake wanaosema kwamba wanaume wao wanataka kuiga wanayoonakatika hizo filamu.

Mmoja wao, Mariam Musabyimana ambaye ni mshauri wa mambo ya afya kijijini ameeleza hili suala linajulikana wilaya nzima na kuwa wameisha anzisha mikakati ya kutoa suluhisho.

“Nilimkuta muatihiriwa  wa hizi filamu za uchi. Ni mwanamke ambaye mumewe  alikuwa akifanya mapenzi kupitia mkundu. Hili limuathiri alipokuenda hospitalini kuzaa mtoto.” Mariam ametangaza

Afisa kwa  wa Kamati ya wanawake nchini wilayani  Nyaruguru, Kamanzi Xaveline ametangaza aliwahi kumpa huduma mwanamke aliyekuwa na matatizo asili ya kuangalia filamu za uchi.

“ Nilikutana na hili suala, mwanamume alikuja na kumuambia mke wake watafanya mapenzi kama wafanyavyo mbwa. Mwanamke alikuwa na machozi sana” Xaveline amesema

Mkurugenzi katika Profemme Twese Hamwe kwa wajibu wa kupambana na unyanyasaji, Frère Wellars amehakikisha hili tatizo lipo na wanatafuta namna ya kulisuluhisha vilivyo.

Ati “Haina budi kuwazindua watu kwani wanaangalia hizo filamu wakiwa chumbani. Tunaomba msaada polisi kupiga marufuku uchuuzi wowote wa hizi filamu”

Takwimu za Porn hub kuhusu raia wanaoangalia filamu za uchi

Kwa mujibu wa Pornhub, Rwanda inajitokeza kwenye nafasi ya 29 barani Afrika kuwa na idadi ya raia wanaoangalia filamu za uchi hasa juma pili na siku nyingine za kupumzika.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.