kwamamaza 7

Kombe la mabara laendelea huku mikasa ya VAR ikijitokeza kwa wingi

0

Katika kombe la mabara ambalo limeanza jumamosi tarehe 18 huku russia ikiwachapa Australia bao 2-0 kwenye siku ya kwanza.

Juma pili hii ambako kulipigwa mechi mbili,ndipo ilipotokea ubishi na malamiko kuhusu mfumo mpia wa fifa wa Uamuzi wa Marefa Unaotegemea Videwo( Video Assistant Referee) ambao ni majaribio ya kwamba utaweza kutumiwa katika kombe la dunia la Urusi mwaka 2018.

Katika mechi ya kwanza ya jumapili iliyowakutanisha Portugal na Mexico kumekuwa na ubishi kama huu ambapo kwenye dakika ya 21 Cristiano alipiga free-kick iliyogonga mwamba na mpira kumkuta Pepe ambaye aliumaliza wavuni na bao likakataliwa kwa sababu ya hii teknolojia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwenye mechi iliyofuata kati ya Chile na Kameruni ilikuwa ni ya kiteknolojia mno ambapo kulitokea mikasa mingi kufuata uamuzi wa aina hii. Dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza ambapo Eduardo Vargas amepiga mkwajuu uliompitia Fabrice Ondoa wa Kameruni huku watu wakishangilia goli uamzi wa tekinolojia huu ukaonyesha kuwa kumekuwa na Offside na bao likakataliwa.

Kumetokea na mkasa mwingine kwenye dakika za mwisho ambapo Sanchez alipiga mkwajuu mkali ambao uliokolewa na Vargas akaumaliza wavuni. Wakati watu walidhania kuwa offside bao lilikubaliwa mwishowe na kuifanya mbili kwa bila.

Katika mwisho wa mechi hii watu walionyesha kutofurahia teknolojia hii akiwemo Santos kochi wa Portugal.

Aidha washabiki waliipa majina mengi teknologia hii kwenye mtandao wa kijamii twitter:

VAR – Video Assisted Rubbish : Videwo ya kutegemea uchafu
VAR – Very Advanced Retardation: Kukawia kulikoendelea

Matokeo ya mechi zilizofanyika yalikuwa:

Urusi 2-0 New Zealand

  1. Boxall (OG) 31’

F,Slomov(G) 69’

-Portugal 2-2 Mexico

Ricardo Quaresma 34’

42’Javier Hernandez

Cedric Soares 86’

90+1’H.Moreno

-Kameruni 0-2 Chile

81’A.Vidal

90+1’E.Vargas

Na mechi ambayo itapigwa hii leo ni kati ya Australia vs Ujerumani.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.