kwamamaza 7

Klabu 10 zenye thamani kubwa Ulaya zinaongozwa na MAN U

0

Kulingana na orodha kutoka utafiti wa Kampuni ya KMPG, Manchester United ya Uingeleza ndio inayoongoza klabu hizi ikiwa na thamani ya bilinioni 3.

Katika utafiti huo uliozingatia vigezo mbali mbali vikiwemo umarufu wa timu, uwezo wa kimchezo, haki za kufanya matangazo ,faida ya kibiashara na hata umiliki wa uwanja inatawaliwa na Manchester United, Real Madrid ya Pili na FC Barcelona tatu.

Hata hivyo miongoni mwa klabu 10 zinazoongoza , timu kutoka ligi ya premia ya Uingeleza ndizo zimeshika nafasi nyingi zikiwa 6.

Kuimarika kwa matangazo ndiko kulifanya klabu za Uingeleza kutawala ordha hiyo ,miongoni mwa timu 32 ambazo zilifanyiwa utafiti thamani ya timu tanu za uingeleza inajumlisha 10.2 Euro bn ambayo ni sawa 42% ya thamani jumla ya timu 32.

Thamani ya timu za Uhispania nayo imeongezeka kupitia kuimarika viwanjani na hii inatokea ya kwamba ndizo zilizokuwa mabingwa wa ulaya kwa kipindi cha miaka tatu iliyopita zikishinda Europa ligi na Hata Champions league, timu hizi zikiwemo Real Madrid na FC Barcelona,ambazo zinashika nafasi katika 10 bora, zinajumlisha 6,6 Euro bn.

Orodha hii ambayo imetawaliwa hususani na timu kutoka ligi tano bora za ulaya inaonyesha kuwa timu za Italia ambazo zimekuwa zikiongoza kutoka miaka ya 1990 zimeshukuka kitamani, Inter Milan ikiwa ndio timu ilyoweza kuibuka mabingwa Ulaya hapo 2010 na Juventus yenye tamani ya 1 Euro bn ikiwa ndio timu pekee inayojaribu kufanya vizuri ikiwa imeweza kufika fainali hivi karibuni. Timu za Italia zinajumlisha thamani ya 3.1 Euro bn ambayo iko sawa na 70% pungufu na tamani ya timu za Uingereza. Ambazo zinafuatia klabu za Ujerumani zenye tamani ya 3.5 Euro bn.

Timu sizohesabiwa kutoka ligi tano bora zilizowahi kupatikana kwenye Ordha hii ni pamoja na(AFC Ajax, PSV Eindhoven, SL Benfica, FC Porto, Fenerbahçe SK and Galatasaray SK) na thamani ya 5% ya orodha nzima.

Hii hapa orodha ya timu 10 bora kithamani

 

  1. Manchester United -Euro 3.0bn
  2. Real Madrid – Euro2.97bn
  3. Barcelona – Euro2.76bn
  4. Bayern Munich – Euro2.15bn

5.Manchester City – Euro1.62bn

6.Arsenal – Euro1.7bn

7.Chelsea – Euro1.5bn

8.Liverpool – Euro1.33bn

9.Juventus – Euro1.01m

10 Paris –Saint Germain FC Euro 843 m

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy’/bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.