kwamamaza 7

Kiwanda cha  sigara cha familia ya Rwigara chaishtaki  serikali ya Rwanda

0

Kiwanda cha sigara cha familia ya marehemu Assinapol Rwigara,Premier Tobacco, kimeishtaki bodi kuu ya kodi(RRA) juu ya kutaifisha baadhi ya vifaa vya msingi vyake,jambo lililozuia kuendeela na kazi zake wakati wa miezi saba.

Mwanasheria wa kiwanda Tobacco Premier,Janvier Rwayitare ameambia mahahakama ya kiuchumi ya Nyarugenge kwamba utaifishaji wa hivi vifaa ulisababisha hasara kubwa na kwa hiyo hili ni suala ambalo linahitaji kutatuliwa haraka.

Pia Janvier Rwayitare amesema kwamba serikali ilitaifisha pia akaunti za benki,hati za usimamizi wa mali na bidhaa zilizomaliza kutayarishwa.

Huyu mwanasheria amependekeza mahakama kutondoa hivi vipingamizi ili  kiwanda kiendelee na kazi zake.

Taarifa za BBC  zimeeleza kuwa upande wa RRA kupitia wanasheria wake,Clement Gatera na Bajeni Byiringiro wamekanusha ombi la upande wa Premier tobacco kwa kueleza kuwa vifaa vilivyotaifishwa haviwezi kukomesha kazi za kiwanda,jambo lilizousha kelele mahakamani.

Pengine wanasheria wameeleza kuwa vifaa vilitaifishwa kwa kuwa kulikuwepo kukwepa kulipa kodi.

Mwanasheria Janvier Rwayitare amekanusha madai haya kwa kuuliza namna ambavyo kiwanda kinaweza kufanya kazi bila vifaa vya msingi,vitabu vya usimamzi wa mali na kaunti za benki.

Kiwanda cha sigara Premier Tobacco kilikuwa kikipatia ajira watu karibu 200.

Bonyeza BWIZA TV kupata habari  na nyimbo mpya

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.