kwamamaza 7

Kivu ya Kaskazini: Gavana Paluku yatangaza tishio la vita vipya kuibuka

0

Mashambulizi ya hapa na pale ya makundi ya waasi katika Kivu ya Kaskazini yanaashiria, Kwa mjibu wa Gavana wake Julien Paluku, vita vikali vinavyoweza kujitokeza kwa mara nyingine eneo hilo.

Yeye anasema mashambulizi haya si kutokea kwa na makundi ya waasi ya nyumbani tu.

Kwa mjibu wa habari alizoitangazia redio Okapi amesema kuwa anatahadhalisha uongozi wa kijeshi, ambapo anasema yanayojitokeza eneo la Beni ni zaidi ya uelewa wa makundi ya waasi, na kwa hivyo jeshi halina budi kuichua mikakati ya kujilinda vita vinavyoweza kuibuka katika eneo hilo.

Aliendelea kusema kwamba mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni anaweza kufanya mtu kufikiri kwamba ni makundi ya waasi wa nyumbani wakati kuna vita vikali vinavyokaribia kuibuka. Hapa alitoa mfano wa waasi walioshambulia eneo la Kabasha, Kasindi na Beni, alisema kwamba waasi hawa walisimama vikali dhidi ya majeshi wa serikali tofauti na vile ilivyo kawaida.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hapa aligusia mashambulizi yanatekelezwa katika maeneo mbalimbali na kwa wakati mmoja. Hili linaashilia nguvu za waasi hao kwa mabomu na silaha kali wanazotumia, wakati ambapo wa mai-mai hawana uwezo wa kutekeleza mashambulizi mahali tofauti na kwa wakati mmoja.

Kumekuwa kukiripotiwa mashambulizi tofauti katika eneo hili la Kivu ya Kaskazini likiwakutanisha makundi ya waasi na majeshi ya serikali.

Na mnamo siku 10 zilizopita ,kuna mwanaumme aliyesema ni msemaji wa kundi lisilotambulika bado, alikiri kwamba ndio wanaopambana na jeshi la serikali katika mashambuizi yanayotokea katika eneo hilo la Kivu ya Kaskazini. Mume huyu anayeitwa John Mangaiko ni kutoka kundi lake linaloitwa Mouvement National pour la Révolution (MNR).

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.